Skip to main content

BIMA YA AFYA KUZINUFAISHA KAYA 26,377 GEITA

Mkuu wa Mkoa wa Geita, Alexander Mnyeti amevitaka vituo vya kutolea huduma za afya vya umma na binafsi kuheshimu na kutoa huduma stahiki kwa wanufaika wa bima ya afya kwa wote.

BIMA YA AFYA KUZINUFAISHA KAYA 26,377 GEITA
Studio Narration JAMBO FM

BIMA YA AFYA KUZINUFAISHA KAYA 26,377 GEITA

0:00 --:--

Mkuu wa Mkoa wa Geita, Alexander Mnyeti amevitaka vituo vya kutolea huduma za afya vya umma na binafsi kuheshimu na kutoa huduma stahiki kwa wanufaika wa bima ya afya kwa wote.

Mnyeti ametoa maagizo hayo katika hafla ya uzinduzi wa Awamu ya Pili ya Mpango wa Bima ya Afya kwa wote mkoani humo iliyofanyika katika Mamlaka ya Mji Mdogo wa Katoro akisema wanufaika wa bima ya afya kwa wote wanayo haki ya kupata huduma wanayostahili kwa mjibu wa mashariti ya bima na taratibu zilizowekwa na serikali na siyo vinginevyo.

“Hairuhusiwi mwananchi kunyimwa huduma kwa sababu zisizo halali, malalamiko yanayojitokeza yashughulikiwe kwa haraka na weledi”, aliagiza Mnyeti.

Aidha aliitaka Ofisi ya Mganga Mkuu wa Mkoa kufuatilia malalamiko kadhaa yanayodai vituo vya kutolea huduma za afya vinatoa kipaumbele kwa wenye fedha taslimu na kupuuza wenye bima.

“Niwaombe sana watoa huduma siyo anapewa kipaumbele anayelipa fedha taslimu na mwenye bima ya afya anapuuzwa kwa sababu hatoi fedha taslimu”, alisema Mnyeti.

Mnyeti aliagiza wakuu wa wilaya, wakurugenzi wa halmashauri na watendaji kuhakikisha wananchi wanapata elimu kuhusu umuhimu, faida, gharama na taratibu za kujiunga na bima.

Alielekeza kila halmashauri ifuatilie, kufanya tathimini na kuwasilisha taarifa kwa wakati baada ya siku 14 ili kubaini mafanikio, changamoto na hatua za kuboresha utekelezaji.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Geita, Dk Omari Sukari alisema mkoa una watoa huduma za afya takribani 5,000 ambao watasaidia kutoa huduma kwa kila mtu ikiwemo wanufaika wa bima.Alisema tayari mkoa umekamilisha kufunga mifumo ya kielektroniki inayosomana na mfumo wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kuongeza ufanisi wa mpango wa bima ya afya kwa wote.

Meneja wa NHIF mkoa wa Geita, Sophia Kaku alisema katika awamu ya pili ya Mpango wa Bima ya Afya kwa Wote mkoa umelenga kusajili kaya 26,377 zenye jumla ya wanufaika 93,157.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.