Skip to main content

BILIONI 441 KUJENGA CHUO MAHIRI CHA TEHAMA DODOMA

Tanzania inatarajia kupata Chuo Mahiri cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (DTI) jijini Dodoma, ambacho ujenzi wake unatarajiwa kugharimu zaidi ya shilingi bilioni 441, kupitia mkopo nafuu kutoka Serikali ya Korea Kusini, kwa ajili ya kuimarisha uzalishaji wa wataalamu wenye ujuzi wa hali ya juu katika teknolojia za kidijiti, ikiwemo Akili Unde.

BILIONI  441 KUJENGA CHUO MAHIRI CHA TEHAMA DODOMA
Studio Narration JAMBO FM

BILIONI 441 KUJENGA CHUO MAHIRI CHA TEHAMA DODOMA

0:00 --:--

Tanzania inatarajia kupata Chuo Mahiri cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (DTI) jijini Dodoma, ambacho ujenzi wake unatarajiwa kugharimu zaidi ya shilingi bilioni 441, kupitia mkopo nafuu kutoka Serikali ya Korea Kusini, kwa ajili ya kuimarisha uzalishaji wa wataalamu wenye ujuzi wa hali ya juu katika teknolojia za kidijiti, ikiwemo Akili Unde.

Mradi huo utaanza kutekelezwa baada ya Serikali ya Tanzania na Benki ya Exim ya Korea Kusini, Novemba 3 mwaka huu, kutia saini mkataba wa mkopo wenye riba nafuu wa dola za Marekani milioni 167.4, sawa na sh. bilioni 441.12, utakaotolewa kupitia Mfuko wa Ushirikiano wa Maendeleo ya Kiuchumi wa Korea (EDCF).

Akizungumza katika hafla ya utiaji saini mkataba huo, Jijini Dar es Salaam Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-Maamry Mwamba, alisema chuo hicho kitakuwa na mchango mkubwa katika kuandaa na kukuza wataalamu wenye ujuzi wa hali ya juu katika fani za kiufundi na kuimarisha sekta ya tehama nchini.

Alisema chuo hicho kitakuwa na vituo vya kisasa vya mafunzo, maabara, miundombinu ya kidijiti na tafiti, huku kikiimarisha uhusiano kati ya taasisi za elimu na sekta ya viwanda ili kupunguza pengo la ujuzi na kuchochea maendeleo ya teknolojia.

“Mradi huu umekuja wakati mwafaka ambapo Tanzania inaendelea kutekeleza ajenda ya mageuzi ya kidijiti na kujenga rasilimali watu pamoja na uwezo wa kitaasisi unaohitajika kushiriki kikamilifu katika uchumi wa kidijiti’ Alisema Dkt. Mwamba.

Alisema Wizara ya Fedha itashirikiana kwa karibu na Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari pamoja na taasisi zote zinazohusika na utekelezaji wa mradi huo, ikiwemo kutoa mchango wa ndani unaohitajika ili kuhakikisha unatekelezwa kwaufanisi.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji Mwandamizi wa Benki ya Exim ya Korea, Bw. Dong-Hoon Lee, alisema mradi huo una umuhimu mkubwa kwa nchi hizo mbili kwa kuwa ni mradi wa kwanza wa EDCF kuidhinishwa mwaka huu na wa kwanza unaohusisha usaidizi katika eneo la Akili Unde.

Alisema majadiliano ya kuidhinisha mradi huo yalianza Aprili mwaka huu kisha ikatolewa sera ya usaidizi wa serikali Agosti mwaka huu Wizara ya Fedha

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.