Skip to main content

BILIONI 204.7 KUTUMIKA UTEKELEZAJI MRADI WA UMEME JUA SHINYANGA

Na Eunice Kanumba –Shinyanga.

BILIONI 204.7 KUTUMIKA UTEKELEZAJI MRADI WA UMEME JUA SHINYANGA

Na Eunice Kanumba –Shinyanga.

Waziri wa Nishati,  Deogratius Ndejembi leo Julai 27, 2026  ameshuhudia utiaji saini wa Mradi wa Umeme jua awamu ya pili, utakaozalisha Megawati 100 wenye thamani ya Bilioni 204.7, unaotekelezwa katka kijiji cha Ngunga wilayani Kishapu mkoani Shinyanga, uliosainiwa kati ya Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) na Kampuni za Sagemcom Energy & Telecom SAS na STEG International Services.

Akizungumza baada ya kushuhudia utiaji saini huo, Ndejembi amesema mradi wa Umeme wa Jua wa Kishapu ni sehemu ya mkakati wa Serikali wa kuimarisha mseto wa vyanzo vya uzalishaji wa umeme (energy mix), kwa lengo la kuongeza upatikanaji wa umeme wa uhakika, wa gharama nafuu na unaotokana na vyanzo vya nishati jadidifu.

Amesema, mradi huo utachangia kuongeza uzalishaji wa umeme kutoka vyanzo vya nishati jadidifu, na kwamba unakwenda  kuimarisha uthabiti wa mfumo wa umeme nchini na kusaidia Serikali kufikia malengo ya kuhakikisha Tanzania inakuwa na umeme wa kutosha kukidhi mahitaji ya sasa na ya baadaye.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO),  Lazaro Twange amesema, kusainiwa kwa mkataba wa ujenzi wa Mradi wa Umeme wa Jua wa Kishapu Awamu ya Pili wenye uwezo wa kuzalisha megawati 100 ni hatua muhimu katika utekelezaji wa mkakati wa TANESCO wa kuongeza uzalishaji wa umeme kupitia vyanzo vya nishati jadidifu.

"Mheshimiwa  Waziri mradi huu wenye thamani ya shilingi bilioni 204.7 utaongeza uimara wa Gridi ya Taifa, kuboresha upatikanaji wa umeme wa uhakika kwa wananchi na sekta za uzalishaji, pamoja na kuchangia utekelezaji wa Dira ya Taifa ya maendeleo nipende kuahidi kuwa TANESCO tutasimamia kwa karibu utekelezaji wa mradi huu ili ukamilike kwa wakati, kwa ubora na kwa kuzingatia viwango vyote vya kitaalamu," amesema  Twange.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mboni Mhita, amesema utekelezaji wa Mradi wa Umeme wa Jua wa Kishapu Awamu ya Pili unaonesha imani kubwa ambayo Serikali ya Awamu ya Sita imeendelea kuwa nayo kwa Mkoa wa Shinyanga kutokana na mazingira mazuri ya uwekezaji na ushirikiano wa wananchi.

Aidha, amebainisha kuwa Serikali ya Mkoa itaendelea kutoa ushirikiano kwa TANESCO, mkandarasi na wadau wote wa mradi ili kuhakikisha utekelezaji wake unakwenda kwa wakati, huku akiwahimiza wananchi kuendelea kulinda miundombinu ya umeme kwani ni rasilimali muhimu kwa maendeleo ya Taifa na ustawi wa vizazi vya sasa na vijavyo.

Teknolojia ya umeme wa jua ni miongoni mwa teknolojia zinazotumia nishati safi na rafiki kwa mazingira, Teknolojia hii hutumia mionzi ya jua kupitia paneli maalumu za sola, ambazo hubadilisha mwanga wa jua kuwa umeme kwa ajili ya matumizi mbalimbali, ikiwemo majumbani, shule, vituo vya afya na shughuli za biashara.

Matumizi ya umeme wa jua husaidia kupunguza utegemezi wa vyanzo vya nishati vinavyoweza kuchafua mazingira, huku ukirahisisha upatikanaji wa umeme katika maeneo ambayo hayajaunganishwa na gridi ya taifa. Hivyo, jamii inahimizwa kutumia teknolojia hii kwa ajili ya nishati endelevu na maendeleo ya kiuchumi.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.