Skip to main content

BILIONI 1.8 KUBORESHA MIUNDOMBINU SHULE ZA MSINGI RORYA, MARA

Na Adam Msafiri, Rorta - Mara.

BILIONI 1.8 KUBORESHA MIUNDOMBINU SHULE ZA MSINGI RORYA, MARA

Na Adam Msafiri, Rorta - Mara.

Serikali imetoa shilingi bilioni 1.8 kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya elimu katika shule za msingi Wilayani Rorya, Mkoa wa Mara, ikiwa ni sehemu ya jitihada za kuimarisha mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji.

Akizindua rasmi madarasa mawili katika Shule ya Msingi Nyahembwe, Mkuu wa Wilaya ya Rorya, Dkt. Khalfan Haule, amesema fedha hizo zinatekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ya elimu ikiwemo ujenzi wa zaidi ya madarasa 50 pamoja na miundombinu mingine muhimu inayolenga kuboresha huduma za elimu kwa wanafunzi.

Dkt. Haule amesema uwekezaji huo ni sehemu ya dhamira ya serikali ya kuhakikisha wanafunzi wanapata elimu katika mazingira bora na salama, huku akisisitiza usimamizi mzuri wa miradi hiyo ili fedha zilizotolewa ziweze kuleta matokeo yaliyokusudiwa.

Kwa upande wake, Afisa Elimu wa Kata ya Mirare, Kilunga Shalaha, amesema kata hiyo imepokea zaidi ya shilingi milioni 100 zinazotumika kujenga madarasa mapya na matundu ya vyoo, hatua ambayo itasaidia kupunguza changamoto ya upungufu wa miundombinu ya elimu na kuongeza ubora wa mazingira ya kujifunzia.

Baadhi ya wananchi wa Wilaya ya Rorya wameipongeza serikali kwa kuendelea kuwekeza katika sekta ya elimu, wakisema hatua hiyo imekuja kwa wakati muafaka katika kukabiliana na changamoto ya uhaba wa madarasa iliyokuwa ikiathiri baadhi ya shule.

Hata hivyo, wananchi hao wameiomba serikali kuelekeza nguvu zaidi katika kuboresha miundombinu ya barabara, wakieleza kuwa hali ya barabara katika baadhi ya maeneo bado ni changamoto inayokwamisha shughuli za kijamii na kiuchumi.

Serikali imeendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo katika sekta ya elimu nchini kwa lengo la kuongeza upatikanaji wa huduma bora za elimu na kuimarisha mazingira ya kujifunzia kwa wanafunzi wa ngazi zote.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.