Mkuu wa usalama wa Iran, Mohsen Rezaei amesisitiza kuwa Mlango wa Bahari wa Hormuz utaendelea kufungwa, hadi pale matakwa yote ya Tehran yatakaposikilizwa na kutekelezwa.
Kauli Razaei inakuja wakati ambapo Tehran inaendelea kusubiri majibu ya mwisho kutoka Washington, kuhusu mapendekezo ya kumaliza vita.

Hata hivyo, Iran imesisitiza kuwa njia hiyo muhimu ya meli itafunguliwa iwapo matakwa yake yote saba yatatekelezwa ikiwemo kuachiwa kwa fedha zake zinazoshikiliwa.
Mzozo huo wa mashariki ya kati, unaendelea kurikisa huku ukisababisha gharama za maisha kupanda kutokana na mfumuko wa bei unaosababishwa na kuadimika kwa mafuta.
Discussion
Reader comments
0 contributions