Skip to main content

BIL. 1.8 ZATUMIKA ULIPAJI FIDIA WANANCHI WALIOPISHA MRADI EACOP SHINYANGA, USAFIRISHAJI MAFUTA NI JANUARI 2027

Na Eunice Kanumba – Shinyanga.

BIL. 1.8 ZATUMIKA ULIPAJI FIDIA WANANCHI WALIOPISHA MRADI EACOP SHINYANGA, USAFIRISHAJI MAFUTA NI JANUARI 2027

Na Eunice Kanumba – Shinyanga.

Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP), hadi sasa umelipa jumla ya shilingi bilioni 35.6 kama fidia kwa wananchi 10,144 kati ya 10,223 sawa na asilimia 99.5 ya wananchi wote walioguswa na zoezi la fidia kwa kupisha mradi huo, ambapo Mkoani Shinyanga kiasi cha Bil. 1.8 zimelipwa kwa walistahili.

Hayo yameelezwa na Mratibu wa Utekelezaji wa Mradi wa EACOP, Jumanne Mohamed Said kutoka Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), katika warsha ya Waandishi wa Habari wa mkoa wa Shinyanga  iliyofanyika Septemba 4, 2026 kwa lengo la kuwajengea uwezo masuala yahusuyo gesi na mafuta.

Mratibu wa Utekelezaji wa Mradi wa EACOP, Jumanne Mohamed Said.

Akizungumzia mradi huo wa bomba la mafuta ghafi Saidi amesema utakapokamilika utakuwa na uwezo wa kusafirisha mapipa 216,000 ya mafuta ghafi kwa siku na unatarajiwa kufanya kazi kwa kipindi cha miaka 25 na utaanza rasmi kusafirisha mafuta ghafi Januari 15, 2027, huku utekelezaji wake ukiwa mbioni kukamilika, kwani umefikia asilimia 87.7.

Katika mkoa wa Shinyanga, mradi huo umepita Wilayani Kahama, ambapo katika kata nane zenye  vijiji saba na mitaa tisa, ambapo kwa ujumla wake kiasi cha shilingi bilioni  1.8 zililipwa kama fidia kwa waliopisha mradi katika kilomita 54 za manispaa hiyo.

Sehemu ya Waandishi Habari waliohudhuria warsha hiyo.

Awali, akifungua warsha hiyo Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga, David Lyamongi amesema, ukamilikaji na kuanza kwa mchakato wa kusafirisha mafuta ghafi kitakuwa ni kichocheo kikubwa cha uchumi na kuimarika kwa pato la Mwananchi mmojammoja, hususan maeneo litakapopita bomba hilo katika manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga.

Lyamongi, pia amewataka wanachi katika maneneo yote lilipopita bomba hilo kulitunza na kuwa walinzi wa miundo mbinu ya bomba la kusafirisha mafuta ghafi ili liweze kudumu na kunufaisha vizazi vya sasa na vijavyo.

Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga, David Lyamongi.

Mradi wa EACOP, unaanzia Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Chongoleani mkoani Tanga, Tanzania, ukiwa na urefu wa jumla ya kilomita 1,443. Kati ya urefu huo, kilomita 1,147 zipo Tanzania na kilomita 296 zipo nchini Uganda.

Mradi huo unatarajiwa kuwa na uwezo wa kusafirisha mafuta ghafi kutoka Uganda hadi katika Bandari ya Chongoleani kwa ajili ya kusafirishwa kwenda katika masoko ya kimataifa.

"Waandishi wa Habari wana nafasi muhimu katika kuelimisha jamii." - Maria Msellem.

Akizungumzia masuala ya nishati katika warsha hiyo, Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano kutoka, TPDC, Maria Msellem, amesema Tanzania inajivunia uwepo wa gesi asilia katika mikoa  ya Lindi na Mtwara na kwamba gesi baada ya kugundulika tayrai imeshaanza kutumika katika baadhi ya maeneo  ikiwemo Mtwara, Lindi na Dar es Salaam.

Msellem amesema pamoja na uwepo wa matumizi ya gesi asilia katika maeneo hayo, bado wananchi wengi hawana uelewa wa kutosha kuhusu matumizi ya nishati hiyo, hivyo kuna umuhimu wa kuendelea kutoa elimu kwa jamii ili wananchi waweze kuelewa matumizi sahihi na salama ya gesi asilia pamoja na fursa na manufaa yanayopatikana kutokana na rasilimali hiyo.

Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano kutoka, TPDC, Maria Msellem.

Amesisitiza kuwa Waandishi wa Habari wana nafasi muhimu katika kuelimisha jamii kwa kutoa taarifa sahihi kuhusu sekta ya mafuta na gesi, ikiwemo matumizi ya gesi asilia na fursa zinazotokana na rasilimali hizo na namana zinavyotumika katika kupunguza matumizi ya uendeshaji wa viwanda,uendeshaji wa vyombo vya usafiri  pamoja na matumizi ya kupikia.

Mwakilishi wa Jambo FM akiwajibika wakati Warsha hiyo ikiendelea.
picha ya pamoja.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.