Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega, ameliambia Bunge leo kwamba bibi wa miaka 70 mkoani Mwanza amempigia simu leo ili amfkishie salamu za shukrani.
Kwa mujibu wa Waziri Ulega, bibi huyo, Hellen Bogoye, alimpigia simu akishukuru kwamba ujenzi wa Daraja la Magufuli umerahisisha maisha ya wananchi wa Mwanza na mikoa ya jirani.

“Bibi Helena mwenye umri wa miaka 70, amenipigia kuniambia nimfikishie salamu Mhe Rais Samia Suluhu Hassan kuwa sasa hivi kabla hujamaliza kunywa soda, tayari unakuwa umevuka kwenda upande wa pili,” alisema Ulega.
Ulega aliyasema hayo wakati akiwasilisha bungeni hotuba yake ya bajeti kwa mwaka 2026/207 bungeni mjini Dodoma.
Ulega aliomba Bunge liidhinishe kiasi cha shilingi trillioni 2.6 ambapo shilingi trilioni 2.4 zitakuwa ni matumizi ya miradi ya maendeleo na shilingi bilioni 97 kwa matumizi ya kawaida
Discussion
Reader comments
0 contributions