Skip to main content

BEI YA MAFUTA SOKO LA DUNIA YAZIDI KUPAA, CHANZO NI VITA MASHARIKI YA KATI

Bei ya mafuta imeripotiwa kupanda tena kwenye soko la dunia kutokana na athari za moja kwa moja za vita vilivyoanzishwa na Marekani na Israel dhidi ya Iran, ambavyo leo vimeingia siku yake ya 32.

Mapema asubuhi ya Jumanne (Machi 31), pipa moja la mafuta liliuzwa kwa dola 115.17 za Kimarekani ambayo ni zaidi ya shilingi za kitanzania 287,925/= kwenye masoko ya Asia, ikiwa ni muda mchache baada ya meli nyingine ya mafuta kushambuliwa kwenye bandari ya Dubai.

Athari hizi huenda zikaikumba zaidi na Tanzania kwasababu takwimu zinaonesha kuwa kiasi cha asilimia 60 ya mafuta yanayoagizwa kuja Tanzania yanatoka katika nchi za Mashariki ya Kati.

Kwa kipindi cha miezi sita iliyopita Tanzania imeagiza mafuta yake kutoka Nchi za Falme za Kiarabu (37%), India (40%), Saudi Arabia (8%), Oman (8%), Kuwait (4%) na Bahrain (2%).

Kutokana na mabadiliko ya bei ya mafuta kwenye soko la dunia, uwezekano wa bei ya mafuta nchini kwa mwezi Aprili na kuendelea kubadilika ni mkubwa hasa ikitegemea bei zilizotumika kuagizia mafuta ndani ya mwezi Machi.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.