Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), imetangaza kupanda kwa bei kikomo za mafuta ya Petroli, Dizeli, na Mafuta ya taa nchini, hali iliyochangiwa na mzozo wa kisiasa wa Mashariki ya Kati na kuathiri uzalishaji na usafirishaji wa mafuta.
Taarifa iliyotolewa ya EWURA imeeleza kuwa, bei za rejareja kwa jiji la Dar es Salaam Petroli ni Tshs 4,057, Dizeli ni Tshs 4,086, na Mafuta ya taa ni Tshs 4,067 kwa lita huku Mkoani Tanga, bei kikomo kwa lita ya petroli ni Tshs 4,123, dizeli Tshs 4,152 na mafuta ya taa Tshs 4,133.
Kufuatia hali hiyo, EWURA imewataka wafanyabiashara kuzingatia bei kikomo zilizotangazwa, na hatua za kisheria zitachukuliwa kwa yeyote atakayekiuka agizo hilo.





Discussion
Reader comments
0 contributions