Skip to main content

BARABARA YA NJIA NNE MBEYA: TAARIFA ZA UPOTOSHAJI ZAMKERA MAKAMU WA RAIS, ATOA MAAGIZO

Makamu wa Rais, Deogratius Ndejembi, ameonesha kukerwa na taarifa za kupotosha, kuhusu ufunguaji wa barabara ya njia nne mkoani Mbeya, kuwapunguzia adha watumiaji baada ya kufanya ukaguzi wa kushtukiza katika eneo la Kabwe.

BARABARA YA NJIA NNE MBEYA: TAARIFA ZA UPOTOSHAJI ZAMKERA MAKAMU WA RAIS, ATOA MAAGIZO
Studio Narration JAMBO FM

BARABARA YA NJIA NNE MBEYA: TAARIFA ZA UPOTOSHAJI ZAMKERA MA...

0:00 --:--

Makamu wa Rais, Deogratius Ndejembi, ameonesha kukerwa na taarifa za kupotosha, kuhusu ufunguaji wa barabara ya njia nne mkoani Mbeya, kuwapunguzia adha watumiaji baada ya kufanya ukaguzi wa kushtukiza katika eneo la Kabwe.

Ndejembi amechukizwa na kitendo cha Meneja wa TANROADS Mkoa wa Mbeya, Mhandisi Suleiman Bishanga kwa kutoa maelezo ya kupotosha kuhusu kuanza kufungua barabara katika eneo la Mdope mkoani humo.

Aidha, amehoji namna Serikali inavyotoa fedha nyingi bila kuona matokeo yanayolingana na thamani yake, akisisitiza kuwa shilingi bilioni 40 si fedha ndogo kiasi cha kuruhusu uzembe na usimamizi dhaifu.

Makamu wa Rais amemtaka Waziri wa Ujenzi, Masanja Kadogosa, kuhakikisha hatua za uwajibikaji zinachukuliwa kuanzia kwa Meneja wa TANROADS aliyempatia taarifa zisizo sahihi, akisisitiza kuwa serikali haitavumilia watendaji wanaowadanganya viongozi huku wananchi wakiendelea kupata adha ya miundombinu.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.