Skip to main content

BANGI YAMTOKEA PUANI MATEI, ATUPWA JELA MAISHA

Mahakama Kuu ya Tanzania, Divisheni ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, imemhukumu kifungo cha maisha jela Aniseta Kosta Matei (38), mkazi wa Nyarutanga wilayani Morogoro, baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kusafirisha dawa za kulevya aina ya bangi zenye uzito wa kilogramu 102.

Hukumu hiyo ilitolewa na Jaji Magoiga katika kesi ya Uhujumu Uchumi Na. 24215/2024, kufuatia ushahidi uliothibitisha kosa hilo pasipo kuacha shaka.

Kwa mujibu wa hati ya mashitaka iliyowasilishwa mahakamani na timu ya Mawakili wa Serikali wakiongozwa na John Mkony, wakisaidiwa na Magreth Lyimo, Brian Mzava na Pauline Massawe, mshtakiwa alikamatwa Agosti 17, 2024 katika eneo la Mafumbo, Nyarutanga mkoani Morogoro, akiwa anasafirisha kiasi hicho cha dawa za kulevya.

Mshtakiwa alishtakiwa chini ya kifungu cha 15(1)(a)(iii) cha Sheria ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, Sura ya 95 (Marejeo ya mwaka 2019), kikisomwa pamoja na aya ya 23 ya Jedwali la Kwanza na vifungu vya 57(1) na 60(2) vya Sheria ya Uhujumu Uchumi na Makosa ya Kupangwa, Sura ya 200 (Marejeo ya mwaka 2022).

Akisoma hukumu hiyo, Jaji Magoiga alieleza kuwa adhabu hiyo imezingatia uzito wa kosa hilo pamoja na madhara ya dawa za kulevya kwa afya ya jamii na ustawi wa jamii.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.