Skip to main content

BALOZI SHELUKINDO AHIMIZA WATUMISHI KUJENGA UTAMADUNI WA KUFANYA MAZOEZI

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo, amewahimiza watumishi wa Wizara hiyo kujenga utamaduni wa kufanya mazoezi ya viungo mara kwa mara ili kuimarisha afya, kuongeza ufanisi na kuwa na utayari wa kutekeleza majukumu yao ya kila siku.

BALOZI SHELUKINDO AHIMIZA WATUMISHI KUJENGA UTAMADUNI WA KUFANYA MAZOEZI
Studio Narration JAMBO FM

BALOZI SHELUKINDO AHIMIZA WATUMISHI KUJENGA UTAMADUNI WA KUF...

0:00 --:--

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo, amewahimiza watumishi wa Wizara hiyo kujenga utamaduni wa kufanya mazoezi ya viungo mara kwa mara ili kuimarisha afya, kuongeza ufanisi na kuwa na utayari wa kutekeleza majukumu yao ya kila siku.

Ametoa wito huo mara baada ya kushiriki mbio za Capital City Half Marathon 2026, zilizofanyika Novemba 1, 2026, katika viwanja vya Chimwaga jijini Dodoma, zikilenga kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa michezo, afya na mshikamano.

Amesisitiza kuwa afya bora ni msingi muhimu wa utendaji kazi wenye tija, hivyo watumishi wanapaswa kuyafanya mazoezi kuwa sehemu ya maisha yao badala ya kusubiri matukio maalumu ya michezo.

Aidha, amewataka watumishi wote wa Wizara kushiriki kikamilifu katika ratiba ya mazoezi ya pamoja inayofanyika kila Jumanne na Alhamisi, akieleza kuwa utaratibu huo ni fursa muhimu ya kuimarisha afya, kujenga mshikamano na kuongeza ari ya uwajibikaji mahali pa kazi.

Mbio za Capital City Half Marathon 2026 zimewakutanisha washiriki kutoka taasisi mbalimbali za Serikali, sekta binafsi na wananchi, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuhamasisha mtindo bora wa maisha kupitia michezo na mazoezi ya viungo.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.