Skip to main content

BAKWATA SINGIDA WATOA RATIBA KUELEKEA SIKUKUU YA EID EL FITR.

Na Saulo Stephen - Singida.

BAKWATA SINGIDA WATOA RATIBA KUELEKEA SIKUKUU YA EID EL FITR.

Na Saulo Stephen - Singida.

Katika kuelekea Sikukuu ya Eid El Fitr, Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) Mkoa wa Singida limetangaza kuwa Sala ya Eid itaswaliwa kimkoa katika viwanja vya Bombadia Mjini Singida.

Katibu wa BAKWATA Mkoa wa Singida, Omari Muna ametangaza ratiba ya sala hiyo wakati akiongea na Jambo Media Ofisini kwake, kuhusu sherehe za Eid El Fitr, mkoani humo.

Amesema, sala ya Eid itafanyika kuanzia saa 2:00 asubuhi katika eneo hilo la viwanja vya Bombadia na kuwataka waumini wa dini ya Kiislamu katika Mkoa wa Singida kujitokeza kwa wingi, kuhitimisha Mfungo wa mwezi mtukufu wa ramadhan.

Katibu wa BAKWATA Mkoa wa Singida, Omari Muna.

Aidha amebainisha kuwa maandalizi yote muhimu yamekamilika na Mgeni rasmi katika swala hiyo anatarajiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Singida, Halima Dendego.

Hata hivyo, Katibu huyo wa BAKWATA Mkoa wa Singida, ameongeza kuwa siku ya Eid pili kutakuwa na burudani maalum katika uwanja wa Bombadia.

Siku kuu ya Eid El Fitr, inatazamiwa kusherehekewa Machi 21, 2026 kwa kutegemeana na muandamo wa mwezi, pamoja na uthibitisho wa Ofisi ya Mufti Mkuu wa Tanzania, Dkt. Abubakar Ibn Zubeir.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.