Skip to main content

BABATI WAPEWA TANO MATUMIZI NISHATI SAFI YA KUNI POA

Na Afarah Suleiman, Babati - Manyara.

BABATI WAPEWA TANO MATUMIZI NISHATI SAFI YA KUNI POA

Na Afarah Suleiman, Babati - Manyara.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2026, Wazo Mwang'onda ameipongeza Halmashauri ya Mji Babati kwa kuwezeaha matumizi ya Nishati safi ya kuni poa,wakati akizindua mradi wa matumizi ya nishati safi katika shule ya sekondari Nakwa wenye thamani ya Shilingi millioni 12.4.

Aidha amewataka Wananchi kuhamasishana kutumia nishati safi ili kuunga mkono juhudi za Mhe.Rais.Dkt Samia Suluhu Hassan katika kutunza mazingira.

Akisoma taarifa ya utekelezaji wa Afua za lishe Bi. Laurencia Urio Afisa lishe ameeleza kuwa Halmashauri ya Mji Babati imefanikiwa kupunguza utapiamlo mkali kwa Watoto wa chini ya miaka 5 kutoka 32% ya mwaka 2022 na kufikia 24% kwa 2025.

Ameongeza kuwa Halmashauri imenunua mashine ya kuongeza virutubishi katika vyakula vya Wanafunzi yenye thamani ya Shilingi mill 7.2 yenye uwezo wa kuchakata zaidi ya kg 4940 kwa mwezi .

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.