Skip to main content

BABA LEVO CUP MBIONI KURINDIMA KIGOMA

Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini Cryton Chipando maarufu Baba Levo ameanzisha mashindani yenye lengo la kuibua vipaji kwa vijani wa Kigoma mjini.

BABA LEVO CUP MBIONI KURINDIMA KIGOMA
Studio Narration JAMBO FM

BABA LEVO CUP MBIONI KURINDIMA KIGOMA

0:00 --:--

Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini Cryton Chipando maarufu Baba Levo ameanzisha mashindani yenye lengo la kuibua vipaji kwa vijani wa Kigoma mjini.

Mashindano hayo ya soka yanayofahamika kwa jina la BABA LEVO CUP yanatarajiwa kuanza rasmi siku ya Jumapili, huku wapenzi wa mchezo wa soka wakisubiri kwa hamu kuona ushindani na burudani itakayopatikana kupitia michuano hiyo.

Mashindano hayo yanatarajiwa kuwa fursa kwa timu zitakazoshiriki kuonyesha uwezo wao, vipaji vya wachezaji na ushindani wa kusaka ushindi katika kila mchezo ambap mshindi katika mashindano hayo akitarajiwa kupokea kiasi cha shilingi milioni kumi na tano.

Mbunge wa Jimbo Kigoma Mjini akizungmza na waandishi wa habari kuelekea uzinduzi wa mashindano ya Baba Levo CUP, Picha na Tryphone Odace

Mbali na ushindani wa uwanjani, michuano hiyo inatarajiwa kuwaunganisha mashabiki wa soka na kuongeza hamasa ya mchezo huo, huku macho na masikio ya wadau yakielekezwa kwenye maandalizi ya ufunguzi wa mashindano hayo ya jumapili.

Hata hivyo baadhi ya viongozi wa timu zilithibitisha kushiriki mashindano hayo wamesema kuwa mashindano hayo ni sehemu ya vijana kuonyesha vipaji vyao na kuonekana na hatimaye kuchekuliwa na timu ndani ndani na nje ya nchi.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.