Waziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema, huduma ya maji mijini imeendelea kutekelezwa na kusimamiwa na Mamlaka za Majisafi na Usafi wa Mazingira.
Aweso ameyasema leo Mei 5, 2026 wakati akiwasilisha bajeti ya makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2026/2027 Bungeni Jijini Dodoma.
"Wizara imeendelea kuimarisha huduma ya maji na usafi wa mazingira mijini kwa kujenga, kukarabati na kupanua miundombinu ya majisafi na usafi wa mazingira," alisema.

Aweso, ameongeza kuwa, katika mwaka 2025/26, jumla ya miradi 226 ilipangwa kutekelezwa ambapo hadi41 mwezi Aprili 2026, miradi 12 imekamilika.
Vilevile, miradi 214 ipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji ambapo kati ya hiyo miradi 16 imetekelezwa kwa zaidi ya asilimia 95 na imeanza kutoa huduma.
Amesema, katika mwaka 2026/27 Wizara itaendelea kuimarisha usimamizi na uendelezaji wa rasilimali za maji kwa lengo la kuhakikisha usalama wa maji na upatikanaji wa maji kwa shughuli za kijamii, kiuchumi pamoja na ikolojia.
"Katika kufanikisha azma hiyo, Wizara imejipanga kutekeleza vipaumbele mahsusi vitakavyozingatia kuongeza upatikanaji wa huduma ya maji vijijini na mijini, kuimarisha miundombinu ya maji, kuendeleza matumizi bora ya rasilimali za maji, pamoja na kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi," alibainisha.
Ukabilianaji huo utajikita kwenye mpango Kabambe wa Taifa wa Maji na Gridi ya Taifa ya Maji, uvunaji wa Maji ya Mvua, kukamilisha Miradi, kupeleka Maji kwenye Vijiji Visivyo na Huduma, kudhibiti Upotevu wa Maji na huduma ya Maji kwenye Vituo vya Afya na Shule.
Discussion
Reader comments
0 contributions