Skip to main content

ATF, TACAIDS KUSAKA UFADHILI MAPAMBANO DHIDI YA UKIMWI

Serikali imesisitiza dhamira yake ya kuendelea kuzihimiza Serikali za Mikoa na Halmashauri nchini kuhamasisha Utafutataji na matumizi ya fedha kutoka ndani, hususani kutoka sekta binafsi, ili kuimarisha mapambano dhidi ya maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (VVU) nchini.

ATF, TACAIDS KUSAKA UFADHILI  MAPAMBANO DHIDI YA UKIMWI
Studio Narration JAMBO FM

ATF, TACAIDS KUSAKA UFADHILI MAPAMBANO DHIDI YA UKIMWI

0:00 --:--

Serikali imesisitiza dhamira yake ya kuendelea kuzihimiza Serikali za Mikoa na Halmashauri nchini kuhamasisha Utafutataji na matumizi ya fedha kutoka ndani, hususani kutoka sekta binafsi, ili kuimarisha mapambano dhidi ya maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (VVU) nchini.

Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS), Dkt. Adam Mrisho ameeleza hayo jana Jumatano, Septemba 23, 2026, baada ya ziara ya Bodi ya Mfuko wa Udhamini wa mapambano dhidi ya virusi vya Ukimwi nchini, (ATF) iliyofanyika katika Mkoa wa Geita,kwa lengo kukagua shughuli za vikundi vya ngazi ya jamii vinavyotekeleza afua za VVU na kupokea mapendekezo mbalimbali.

Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS), Dkt. Adam Mrisho akizungumza na wananchama wa KONGA wilaya ya Geita,akiwa katika kituo cha Afya Katoro.Picha na (Ibrahim Rojala)

Dkt.Mrisho amesema ushirikiano wa Serikali na sekta binafsi ni muhimu katika kuongeza rasilimali zinazohitajika kupambana na VVU na kueleza kuwa kupitia ziara hiyo, Bodi imejifunza kuwa inapaswa kuendelea kutafuta rasilimali fedha na kusimamia zilizopatikana ili ziweze kutumika kwa malengo yaliyokusudiwa pamoja na kuwajengea uwezo wa kutafuta rasilimali fedha katika sekta binafsi,watumishi na wadau kwa ngazi za Mikoa na Halmashauri nchini.

“Sekta binafsi inachangia karibu asilimia 70 ya kufikia Malengo ya Dira ya Maendelo ya 2050 kwahiyo ni fursa zaidi ambazo tunaziona na kuweza kufanya kazi pamoja na Mikoa ili kuunganisha nguvu za Serikali pamoja na sekta binafsi katika mapambano haya na mwitikio wa VVU na Ukimwi”amesema Dkt Mrisho.

Mratibu wa Kudhibiti Ukimwi Mkoa wa Geita, Dkt. Yohane Kihaga amesema takwimu zinaeleza kuwa Katika mwaka 2026, Mkoa huo unakadiriwa kuwa na takribani watu wapatao 95,100 wanaoishi na Virusi vya UKIMWI.

Aidha amesema hadi kufikia Agosti 2026, Jumla ya WAVIU 78,193 sawa na asilimia 82.22 ya WAVIU wote wanatambua hali zao, kati ya hao, WAVIU wapatao 77,448 sawa na asilimia 99.05 wako kwenye huduma za tiba na matunzo ya ARVs na asilimia 98.83 ya walioko kwenye tiba ya ARVs wamefikia kiwango cha ufubavu wa VVU mwilini (HIV Viral Suppression).

Mratibu wa Kudhibiti Ukimwi mkoa wa Geita, Dkt. Yohane Kihaga akiwasilisha taarifa ya hali ya Maambukizi ya VVU/UKIMWI mbele ya Ugeni wa Bodi ya Mfuko wa Udhamini wa mapambano dhidi ya virusi vya Ukimwi nchini, (ATF).

Kupitia taarifa hiyo Dkt. Kihaga ameeleza kuwa miongoni mwa changamoto zilizopo ni utegemezi mkubwa wa fedha za wadau katika kuwezesha afua za kupambana na VVU/UKIMWI haki iliyoathiri utekelezaji wa afua mbalimbali za VVU hasa afua kinga na tiba ngazi ya jamii zilizofanyika kwa utegemezi mkubwa wa fedha za wadau.

Kwa Upande wake Mwenyekiti wa umoja wa watu wanaoishi na VVU/ UKIMWI Wilaya ya Geita, Faida Mwendesha amesema Baraza la watu wanaoishi na Virusi vya UKIMWI Halmashauri ya Wilaya ya Geita,linaishukuru Serikali kwa kuendelea kutoa ufadhili na huduma za VVU na UKIMWI kwa waviu hata baada ya kupungua kwa ufadhili wa wadau na kuipongeza bodi ya wadhamini ya mfuko wa udhamini wa kudhibiti UKIMWI (ATF) kwa kukutana na KONGA ya Wilaya ya Geita.

Mwenyekiti wa umoja wa watu wanaoishi na VVU/ UKIMWI wilaya ya Geita, Faida Mwendesha akisoma taarifa ya utendaji ya umoja huo mbele ya Bodi ya Mfuko wa Udhamini wa mapambano dhidi ya virusi vya Ukimwi nchini, (ATF),katika kituo cha Afya Katoro.

Nae Katibu Tawala Mkoa wa Geita, Mohamed Gombati ameomba fursa kwa wataalam wa afya Mkoani humo kuendelea kujengewa uwezo hususani kundi la Maendeleo ya Jamii ambalo anaamini kwamba litatoa mchango mkubwa katika makabiliano dhidi ya virusi vya Ukimwi.

“Naamini kwa ujio wenu,kwa kushirikiana tutafungua maeneo mengi ya fursa za namna gani tunaweza kuwasilisha ‘intervesion’ zetu lakini kubwa zaidi mwenyekiti mimi niendelee kukuomba fursa ya kujengewa uwezo waganga wafawidhi wa vituo vyetu na maafisa maendeleo ya Jamii kama kweli tukijenga uwezo wakawa na ‘skills’ mbalimbali zinaweza zikatusaidia”amesema Gombati.

Katibu Tawala Mkoa wa Geita, Mohamed akizungumza na wageni kutoka Bodi ya Mfuko wa Udhamini wa mapambano dhidi ya virusi vya Ukimwi nchini, (ATF),baada ya ugeni huo kufika ofisini kwake Septemba 23,2026.

Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Udhamini wa Kudhibiti UKIMWI (AIDS Trust Fund - ATF) Sabasaba Moshingi ameeleza kuwa kutokana na kukauka kwa fedha za ufadhili kutoka kwa wahisani ni wakati wa kugeukia ubunifu kupitia ushirikishwaji wa Taasisi zilizopo ndani ya jamii kama vile Benki na kuangalia umuhimu wa kutambua wadau muhimu wa kushirikiana nao katika hilo wakiwemo wachimbaji wa madini.

Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Udhamini wa Kudhibiti UKIMWI (AIDS Trust Fund - ATF), Sabasaba Moshingi akizungumza na wanachama wa KONGA wilaya ya Geita katika Kituo cha Afya Katoro.

Aidha amepongeza hatua ya Halmashauri ya Wilaya ya Geita kutenga kiasi cha Shilingi 22,200,000/zilizotumika kuwasomesha katika chuo cha ufundi (VETA) Geita Manispaa, kwa kuwagharamikia kwa kulipia kila kitu isipokuwa fedha kwa ajili ya matumizi madogo madogo vijana 20 wanaoishi katika mazingira magumu ambao kati yao vijana 9 ni WAVIU na vijana 11 wanatoka katika kaya za WAVIU wazazi/ walezi wao na baadhi yao wanatoka katika kaya za walengwa wa TASAF.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.