Skip to main content

ANGOLA YAFUNGUA FURSA ZA UWEKEZAJI, BIASHARA NA TANZANIA

Rais wa Angola, João Lourenço, amesema nchi yake inalenga kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na Tanzania kwa kuongeza biashara na uwekezaji baina ya mataifa hayo.

ANGOLA YAFUNGUA FURSA ZA UWEKEZAJI, BIASHARA NA TANZANIA
Studio Narration JAMBO FM

ANGOLA YAFUNGUA FURSA ZA UWEKEZAJI, BIASHARA NA TANZANIA

0:00 --:--

Rais wa Angola, João Lourenço, amesema nchi yake inalenga kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na Tanzania kwa kuongeza biashara na uwekezaji baina ya mataifa hayo.

Akizungumza Ikulu jijini Dar es Salaam, Rais Lourenço amesema licha ya uhusiano wa kihistoria na kidugu uliopo kati ya Angola na Tanzania kuna umuhimu wa kuimarisha zaidi ushirikiano wa kiuchumi ili kuchochea maendeleo ya nchi hizo na kuboresha maisha ya wananchi.

Amesema nchi hizo zimesaini mikataba na makubaliano ya ushirikiano ikiwemo katika huduma za usafiri wa anga, hatua inayolenga kurahisisha mawasiliano na safari za wafanyabiashara na wawekezaji pamoja na usafirishaji wa bidhaa.

Aidha, amesisitiza umuhimu wa kuimarisha miundombinu ya usafiri wa anga na majini ili kufungua zaidi fursa za biashara na uwekezaji, akieleza kuwa ushirikiano kati ya serikali na sekta binafsi unaweza kuongeza manufaa ya kiuchumi kwa mataifa hayo.

Rais Lourenço amezitaka nchi za Afrika kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi ndani ya bara hilo ili kutumia fursa zilizopo na kupunguza utegemezi mkubwa wa biashara na uwekezaji kutoka Ulaya, Amerika na Asia.

Rais João Lourenço yupo nchini kwa ziara ya kikazi ya siku tatu inayolenga kuimarisha uhusiano wa kihistoria na kidugu pamoja na kupanua ushirikiano wa kiuchumi, biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Angola.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.