Mtu mmoja, Humphrey Elisamon (63), mkazi wa Hongoro ameuwawa baada ya kujeruhiwa kwa panga kichwani na Dickson Elimringi Msoka (22) ambaye ni mtoto wa mdogonwake na marehemu.
Taarifa ya Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam imeeleza kuwa, tukio hilo limetokea Oktoba, 18, 22026katika eneo la Mungu Mwema Hongoro, lililopo Kibamba Ubungo jijini Dar es Salaam.

"Mtuhumiwa huyo baada ya tukio alishambuliwa na wananchi kabla ya Polisi kufika akiwa katika hali mbaya na baadae alipoteza maisha akiwa anapelekwa hospitali," ilieleza sehemubya taarifa hiyo.
Jeshi la Polisi limeeleza kuwa uchunguzi zaidi juu ya tukio hilo bado unaendelea na limetoa wito kwa wananchi kushirikiana na mamlaka mbalimbali za kijamii, kiuchumi, kisheria na kidini, ili kuzitatua changamoto mbalimbali zinazowakabili.

Discussion
Reader comments
0 contributions