Skip to main content

AMANI NI HAZINA YETU KIUCHUMI, KIJAMII - DKT. SAMIA

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema amani iliyopo nchini ni hazina ya shughuli za kiuchumi na kijamii.

AMANI NI HAZINA YETU KIUCHUMI, KIJAMII - DKT. SAMIA

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema amani iliyopo nchini ni hazina ya shughuli za kiuchumi na kijamii.

Dkt Samia amesisitiza kuwa bila amani, hakuna kujenga uchumi wala hakuna shughuli za kijamii.

Ametoa kauli hiyo leo tarehe 21 Aprili, 2026 katika kongamano la mama na baba lishe lililofanyika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC), Jijini Dar es Salaam.

Rais Dkt. Samia akiwa amevalia Vazi la Kupika wakati wa Kongamano la Kitaifa la Mama na Baba Lishe Tanzania lililofanyika ukumbi wa Julius Nyerere Dar es salaam, Leo Aprili 21, 2026.

“Mmeshuhudia siku tatu zile, hakukuwa na kuchezana, hakuwa na harusi wala ‘kitchen party’, hakukuwa na mimina wala mkusanyiko kwenye bar. Hakukuwa na chochote zilikuwa siku tatu tu…,” amesema Dkt Samia.

Mkuu huyo wa nchi, ametumia jukwaa la kongamano hilo, kuwaomba Watanzania kueindeleza amani ya Taifa.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.