Skip to main content

ALIYEPOKWA UWAZIRI MKUU AUKWAA USPIKA WA BUNGE SENEGAL

Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Senegal, Ousmane Sonko amechaguliwa kuwa Spika wa Bunge la Taifa hilo, akipata kura 132 kati ya kura 133 ziliopigwa na Wabunge.

Hatua hiyo, inaonesha uungwaji mkono mkubwa wa Sonko, kufuatia uchaguzi huo uliofanyika siku chache baada ya Rais Bassirou Diomaye Faye kumuondoa kwenye nafasi yake ya Uwaziri Mkuu.

Ousmane Sonko.

Kabla ya kupigiwa kura kuongoza Bunge, Sonko alirejeshwa rasmi kama Mbunge, hiyo ikiwa ni baada ya aliyekuwa Spika wa Bunge awali, El Malick Ndiaye kujiuzulu, ili kumpisha Sonko.

Bunge la Senegal, ambalo lina Wabunge wengi wanaomuunga mkono Sonko, linatarajiwa kuwa na ushawishi mkubwa katika maamuzi ya Serikali na linaweza kuathiri utendaji kazi wa Raisi Faye.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.