Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma linamshikilia dereva wa Wakala wa Barabara za Vijini na Mijini (TARURA) Wilaya ya Dodoma Sath John Masawa (31) kwa kosa la kumtisha kwa kitu kilichodhaniwa kuwa ni bastola dereva wa basi la la Kmpuni ya SATCO lenye namba za usajili namba T308 EME Said Fadhili (54), wakati akitoka kituo cha kuweka mafuta na kudaiwa kukwangua gari ya TARURA lenye usajili namba STM 5806 aina ya Land Cruseir LX 70 series .
Jeshi la Polisi lilifika eneo la tukio na kumkamata Sath John na baada ya kufanya upekuzi lilifanikiwa kutambua kuwa kitu alichokuwa amevaa kiunoni ni toyi siyo silaha halisi kama ilivyodhaniwa na wananchi na kugundua kuwa gari hilo halikuwa na namba halisi ambazo ni STM 5806 mali ya TARURA bali lilikuwa na namba za usajli T 881 ENZ ambazo ni za gari la mtu mwingine.
Aidha mtuhumiwa huyo anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa mahojiano na hatua zaidi za kisheria na kutoa onyo kwa madereva kuacha kutumia namba bandia za magari kwani kufanya hivyo kunaficha utambulisho halisi wa gari kitendo ambacho ni kosa kwa mujibu wa sheria.
Discussion
Reader comments
0 contributions