Skip to main content

ALIYEMPIGA ASKARI LUGALO NI DAKTARI, MAT WATOA TAMKO

Chama cha Madaktari Tanzania (MAT) kimesema kinafuatilia kwa karibu tukio la Septemba 8, 2026 linalomhusisha Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Ndani katika Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila, Conrad Agonza Kahyoza na Askari wa Usalama Barabarani mwenye namba F.8886 SGT.

Kupitia taarifa yake, MAT imeeleza kuwa, Uongozi wa chama umefanya mazungumzo na Jeshi la Polisi, kupitia Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SACP Murilo na kufahamishwa kuwa Dkt. Agonza alipata majeraha na kupelekwa Hospitali kwa ajili ya matibabu ya dharura, ambapo hali yake kwa sasa imeimarika.

Taarifa hiyo iliyotolewa na Rais wa Chama hicho cha Madaktari Nchini, Dkt. Alex Elifuraha Msoka imefafanua kuwa, Dkt. Agonza anashikiliwa katika Kituo cha Polisi Oysterbay na kwamba wanaendelea kufuatilia ustawi wa wake, ili kuhakikisha anapata huduma stahiki za matibabu wakati wowote atakapohitaji.

Aidha, MAT kupitia Wanasheria wake kinafuatilia taratibu za kisheria kwa lengo la kuhakikisha Mwanachama wake anapata msaada wa haraka wa kisheria, ikiwemo suala la dhamana.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.