Mwanasiasa mashuhuri wa upinzani nchini Guinea, Aliou Bah, aliyekuwa kuwa gerezani kwa tuhuma za kumtukana kiongozi mkuu wa utawala wa kijeshi, Jenerali Mamadi Doumbouya, ameachiwa huru kufuatia msamaha wa rais baada ya kutumikia takribani miaka miwili gerezani.
Hatua hiyo imemweka huru mmoja wa viongozi wakuu wa upinzani katika taifa hilo la Afrika ya Magharibi, wakati ambapo mashirika ya haki za binadamu na wapinzani wa kisiasa wakiutuhumu utawala wa kijeshi chini ya Doumbouya kwa kuzidisha kile wameita “uminywaji wa sauti za wakosoaji” tangu ulipochukua madaraka mwaka 2021.

Kuachiwa huru kwa kiongozi huyo kunakuja kufuatia msamaha wa Rais Doumbouya alioutoa kwa wafungwa 217 kuadhimisha Siku ya Uhuru wa Guinea.
kulingana na agizo la Rais lililosomwa na Katibu wa Rais kwenye televisheni ya taifa , Amara Camara. Jina la Aliou Bah alikuwa miongoni mwa waliofaidika na msamaha huo.
Bah, ambaye ni Mwenyekiti wa chama cha Liberal Democratic Movement (Model), alikuwa ameshikiliwa tangu Desemba 2024 na kuhukumiwa rasmi mwezi Januari mwaka uliofuata.

Alitumikia jela kwa muda wa Miaka 2, huku sababu za kukamatwa kwake na kufungwa gerezani kwa kipindi hicho ni Kutoa kauli za "kudhalilisha na kumtukana" Mkuu wa Nchi

Miongoni mwa kauli hizo ni pamoja na tamko lake la kuwataka viongozi wa dini nchini Guinea "kuvunja ukkimya wao" kuhusu hali ya kisiasa ya nchi hiyo, huku akiutaja utawala wa kijeshi wa National Committee of Rally for Development (CNRD) kuwa "hauwezi wala hauna uwezo wa kuongoza".

Hata hivyo Mahakama ya rufaa ilithibitisha kifungo chake mnamo mei 2025
Sanjari na hilo Kesi yake ilifika hadi katika Mahakama ya Haki ya Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS). Katika barua ya tarehe 25 Septemba, mahakama hiyo ya kanda iliiomba Mahakama Kuu ya Guinea kuamuru kuachiwa huru mara moja na bila masharti kwa mwanasiasa huyo.

Utawala wa Jenerali Doumbouya uliibuka mara baada ya kutwaa madarakani mnamo Septemba 2021 baada ya kumipindua Rais Alpha Condé, aliyekuwa kiongozi wa kwanza kuchaguliwa kwa njia ya kidemokrasia nchini humo.
Doumbouya alizidisha ushawishi na kusimika zaidi uongozi wake baada ya kushinda Uchaguzi wa Urais wa Desemba 2025, uchaguzi ambao haukushirikisha mgombea wowote mkuu kutoka vyama vya upinzani.
Vyama vya upinzani vimeendelea kuwashutumu viongozi wa kijeshi kwa kubana uhuru wa kisiasa kwa mfumo maalum. Vyama kadhaa vikuu vya kisiasa vimefutwa, maandamano yamepigwa marufuku au kutawanywa na vikosi vya usalama, huku wakosoaji wengi wa serikali wakikamatwa, kuhukumiwa, kulazimishwa kukimbilia ukimbizini, au kupotezwa.
Discussion
Reader comments
0 contributions