Skip to main content

ALIYECHIMBA HANDAKI APANDISHWA KIZIMBANI, AKANA MASHTAKA

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza limemfikisha mahakamani Evance Ndeka Bisesagu, mfanyabiashara na mkazi wa Bupumula, Wilaya ya Ilemela, akikabiliwa na mashtaka mawili ya jinai ikiwemo kujenga bila kibali na kufanya ujenzi kwenye eneo la wazi.

ALIYECHIMBA HANDAKI APANDISHWA KIZIMBANI, AKANA MASHTAKA

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza limemfikisha mahakamani Evance Ndeka Bisesagu, mfanyabiashara na mkazi wa Bupumula, Wilaya ya Ilemela, akikabiliwa na mashtaka mawili ya jinai ikiwemo kujenga bila kibali na kufanya ujenzi kwenye eneo la wazi.

​Mshitakiwa huyo amepandishwa kizimbani leo, Juni 16, 2026, mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mwanzo Buswelu, Mhe. Mariam Omary, ambapo alisomewa mashtaka yanayomkabili katika shauri la jinai namba 124 la mwaka 2026.

Katika kosa la kwanza, Bisesagu anashtakiwa kwa kujenga bila kibali, kinyume na kifungu cha 4(1), 4(a)(b), na 5(1) cha Sheria ya Ada na Ushuru ya Manispaa ya Ilemela ya Mwaka 2024.

​Kosa la pili ni kujenga kwenye eneo la wazi, kinyume na kifungu cha 4(B) na 14 cha Sheria ya Ada na Ushuru ya Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela ya Mwaka 2022.

Akisoma shauri hilo, Hakimu Mariam Omary alieleza kuwa mshtakiwa alitenda makosa hayo mnamo Aprili 22, 2026, katika eneo la Bupumula, Kata ya Nyamhongolo, Wilaya ya Ilemela.

​Inadaiwa kuwa mshtakiwa, kinyume cha sheria na kwa makusudi, alikutwa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilemela, Godluck Lukandiza, akiwa amejenga nyumba kwenye eneo la wazi katika Kitalu namba 700, jambo ambalo ni kinyume na sheria za manispaa hiyo.

Baada ya kusomewa mashtaka hayo, mshtakiwa alikana makosa yote. Alipoulizwa na Hakimu kama anao wadhamini, mshtakiwa alijibu kuwa hana wadhamini wa kumdhamini mahakamani hapo.

​Kufuatia hatua hiyo, Hakimu Mariam alimtaka mshtakiwa ajidhamini mwenyewe kwa sharti la kuacha nakala ya kitambulisho chake na kuhakikisha anatimiza masharti ya dhamana kwa kurudi mahakamani hapo tarehe iliyopangwa.

​Kesi hiyo imeahirishwa hadi tarehe Juni 24, 2026, ambapo itakuja tena mahakamani kwa ajili ya Kusikilizwa.

Itakumbukwa kuwa taarifa ya kukamatwa kwa mshtakiwa huyo ilitolewa Aprili 23, 2026 na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, DCP Wilbrod Mutafungwa, wakati alipotembelea eneo hilo kukagua ujenzi na mahandaki yaliyokuwa yamechimbwa na mshtakiwa huyo  yaliyozua taharuki kwa wananchi.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.