Skip to main content

ALAT YASISITIZA UMUHIMU WA USHIRIKIANO KUKUZA UCHUMI WA HALMASHAURI ZA KIGOMA

Na Tryphone Odace, Kibondo – Kigoma.

ALAT YASISITIZA UMUHIMU WA USHIRIKIANO KUKUZA UCHUMI WA HALMASHAURI ZA KIGOMA

Na Tryphone Odace, Kibondo – Kigoma.

Wajumbe wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT), Mkoa wa Kigoma, wametakiwa kuendelea kushirikiana kwa karibu katika kuimarisha maendeleo na kukuza uchumi wa Halmashauri zote za mkoa huo.

Rai hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa ALAT Mkoa wa Kigoma, Alex Baragomwa, wakati wa kikao cha jumuiya hiyo kilichofanyika wilayani Kibondo kwa ajili ya kujadili na kupitia taarifa za utekelezaji wa shughuli za robo ya nne ya mwaka wa fedha 2025/2026.

“Mshikamano na ushirikiano miongoni mwa wajumbe wa ALAT ni muhimu katika kuhakikisha halmashauri zote nane za Mkoa wa Kigoma zinaendelea kupiga hatua katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kukuza uchumi wa wananchi,” amesema Baragomwa.

Kabla ya kikao hicho, wajumbe wa ALAT Mkoa wa Kigoma walifanya ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo.

Miradi iliyotembelewa ni pamoja na Chuo cha Maafisa Tabibu, Soko Jipya la Kisasa la Nane Nane, Jengo la Halmashauri, vibanda vya soko la samaki, pamoja na kikundi cha wajasiriamali cha Kaa Kazi.

Ziara hiyo imelenga kujionea hatua zilizofikiwa katika utekelezaji wa miradi hiyo, pamoja na kutathmini namna inavyoweza kuchangia katika kuboresha huduma na kuongeza fursa za kiuchumi kwa wananchi wa Kibondo.

Aidhawajumbe wa ALAT wameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo kwa ushirikiano unaoendelea katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kuwataka viongozi pamoja na watendaji kuendeleza kasi hiyo.

Mkuu wa Wilaya ya Kibondo, Kanali mstaafu AggreyMagwaza, pamoja na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kibondo, Hamisi Tahiro, wameipongeza ALAT kwa kuendelea kuimarisha ufuatiliaji wa shughuli za maendeleo katika Mkoa wa Kigoma.

Wamesema ufuatiliaji wa karibu wa miradi na shughuli za halmashauri ni muhimu katika kuhakikisha rasilimali zinatumika ipasavyo na wananchi wanapata manufaa yaliyokusudiwa.

Kwa ujumla, kikao na ziara hiyo vimeendelea kusisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya viongozi wa halmashauri, ALAT na wadau wengine katika kuhakikisha miradi ya maendeleo inatekelezwa kwa ufanisi na kuchochea maendeleo ya Mkoa wa Kigoma.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.