Skip to main content

ALAT SINGIDA YATEMBELEA MIRADI YA MAENDELEO IKUNGI IKIPONGEZA UTEKELEZAJI

Kamati ya ALAT Mkoa wa Singida imefanya ziara ya kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika Wilaya ya Ikungi, kwa lengo la kujionea maendeleo ya miradi hiyo na kutathmini utekelezaji wake.

ALAT SINGIDA YATEMBELEA MIRADI YA MAENDELEO IKUNGI IKIPONGEZA UTEKELEZAJI

Kamati ya ALAT Mkoa wa Singida imefanya ziara ya kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika Wilaya ya Ikungi, kwa lengo la kujionea maendeleo ya miradi hiyo na kutathmini utekelezaji wake.

Katika ziara hiyo, kamati imetembelea miradi mitatu ambayo ni Kiwanda cha Kuzalisha Mbegu, Shamba la Mwekezaji linalolijishughulisha na kilimo cha Mbegu pamoja na Ofisi ya Kata ya Mang’onyi.

Aidha, kamati imepata fursa ya kujionea shughuli za uzalishaji wa Mbegu kiwandani pamoja na shughuli za kilimo zinazofanyika katika shamba la mwekezaji, ambazo ni sehemu ya uwekezaji unaochochea ukuaji wa sekta ya Kilimo na Maendeleo ya Uchumi katika Wilaya ya Ikungi.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Mwenyekiti wa ALAT Mkoa wa Singida, Geoffrey Shabani Mdama, ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi kwa juhudi za kuvutia uwekezaji na kutumia fursa zilizopo katika kuchochea maendeleo ya wananchi.

Kamati ya ALAT Mkoa wa Singida.

Amesema Wilaya ya Ikungi imeonesha juhudi katika kuvutia uwekezaji na kutumia fursa zilizopo kwa ajili ya maendeleo, huku akizihimiza Halmashauri nyingine kuiga mfano huo kwa kushirikiana na wawekezaji ili kuhakikisha fursa zinazotumika kuleta maendeleo na kuboresha maisha ya wananchi.

Ameongeza kuwa ushirikiano kati ya Serikali za Mitaa na wadau wa maendeleo ni muhimu katika kuharakisha utekelezaji wa Miradi na kuhakikisha wananchi wananufaika na uwekezaji unaofanyika katika maeneo yao.

Kamati ya ALAT Mkoa wa Singida

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.