Skip to main content

AJIRA KWA WAHITIMU: BULEMBO AVUNJA UKIMYA, SERIKALI YATOA MAJIBU

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba, amesema Serikali inaendelea kulifanyia kazi suala la ajira kwa wahitimu wa vyuo vikuu kupitia hatua mbalimbali za kibajeti, kisera na kiutawala, akieleza kuwa suala hilo ni muhimu kutokana na changamoto inayowakabili vijana wengi nchini.

Dkt. Nchemba ameyasema hayo leo Alhamisi Novemba 05, 2026 wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum kupitia kundi la Vijana, Halima Bulembo, aliyetaka kujua mkakati wa Serikali kuhakikisha mafunzo kwa vitendo yanayotolewa kwa wahitimu yanakuwa daraja la kupata ajira zenye staha na endelevu.

Waziri Mkuu amesema hoja hiyo ni ya msingi na inafanana na hoja binafsi iliyowahi kuwasilishwa na Mbunge Dkt. Selemani Jafo, ambayo Serikali iliipokea na kuanza kuifanyia kazi.

Ameeleza kuwa Serikali itaendelea kulifanyia kazi suala hilo na kutoa taarifa kuhusu hatua zitakazokamilishwa, ikiwemo kutoa maelezo Bungeni pale itakapohitajika.

Katika swali lake, Bulembo amesema takribani asilimia 62 ya wahitimu wa vyuo vikuu nchini hutumia muda mrefu kupata ajira rasmi, akitaka kujua namna Serikali itakavyotekeleza dhamira iliyoainishwa katika Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2025–2030 ya kuwapatia wahitimu mafunzo kwa vitendo kupitia taasisi za umma na sekta binafsi.

Amehoji pia hatua zitakazochukuliwa kuhakikisha waajiri wanatoa fursa hizo na kwamba mafunzo hayo yanawawezesha wahitimu kupata ajira badala ya kuwaongezea uzoefu bila uhakika wa kuajiriwa.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.