Skip to main content

AJALI YAONDOA UHAI WA MPIGA PICHA OFISI YA RC SHINYANGA, SABA WAJERUHIWA WAKIWEMO WAANDISHI WA HABARI

Na Eunice Kanumba – Shinyanga .

AJALI YAONDOA UHAI WA MPIGA PICHA OFISI YA RC SHINYANGA, SABA WAJERUHIWA WAKIWEMO WAANDISHI WA HABARI
Studio Narration JAMBO FM

AJALI YAONDOA UHAI WA MPIGA PICHA OFISI YA RC SHINYANGA, SAB...

0:00 --:--

Na Eunice Kanumba – Shinyanga .

Mpiga picha wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Boaz Martine amefariki dunia huku waandishi wa habari Frank Mshana wa ITV/Radio One na Johnson James wakiwa miongoni mwa watu saba waliojeruhiwa katika ajali ya barabarani iliyotokea Mei 19, 2026 katika Kata ya Samuye, Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga mkoani Shinyanga.

Ajali hiyo ilihusisha gari aina ya Toyota Harrier lenye namba T.210 EDB na Toyota Land Cruiser Hardtop lenye namba DFPA 8920 mali ya shirika la KOICA, lililokuwa limebeba waandishi wa habari pamoja na watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.

Boaz Martine.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Mei 20, 2026, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga SACP Janeth Magomi amesema chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa Toyota Harrier aliyekuwa akijaribu kulipita gari lililokuwa mbele yake bila kuchukua tahadhari, hali iliyosababisha kugongana na Land Cruiser hiyo na kutumbukia mtaroni.

Mbali na Frank Mshana na Johnson James afisa habari ofisi ya mkuu wa Mkoa, majeruhi wengine ni Koplo Swahiba Msangi, Neema Madono (36), Rehema Edson (45), Shadia Omari (32) pamoja na dereva wa Land Cruiser Laurence Peter (34). 

Majeruhi wanaendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, SACP. Janeth Magomi.

Kamanda Magomi ametoa wito kwa madereva kuzingatia sheria za usalama barabarani huku akisisitiza kuwa Jeshi la Polisi litachukua hatua za kisheria dhidi ya madereva watakaobainika kusababisha ajali kwa uzembe.

Aidha kamanda Magomi ameanisha kuwa wanaendelea kumtafuta dereva aliyesababisha ajali hiyo ambaye ametelekeza gari lake na kutokomea kusikojulikana.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.