Skip to main content

AJALI YA MABASI KUGONGANA: WANANE WAAGA DUNIA DODOMA

Na Gideon Gregory - Dodoma.

AJALI YA MABASI KUGONGANA: WANANE WAAGA DUNIA DODOMA

Na Gideon Gregory - Dodoma.

Watu wanane wamefariki dunia na wengine 66 kujeruhiwa kufuatia ajali iliyohusisha mabasi mawili ya abiria yaliyogongana katika Kijiji cha Ibihwa, Wilaya ya Bahi, mkoani Dodoma, kando ya barabara kuu ya Dodoma Singida.

Ajali hiyo imehusisha basi la kampuni ya Isamilo lenye namba za usajili T 428 EXP, lililokuwa likitoka Mwanza kuelekea Dar es Salaam, na basi la Libanika Luxury lenye usajili T 897 DUP, lililokuwa likitoka Dar es Salaam kuelekea Mwanza.

Kwa mujibu wa taarifa, watu Saba wamepoteza maisha papo hapo huku mmoja akipoteza maisha wakati wakipelekwa hospitali kwaajili ya kupatiwa matibabu na majeruhi wakipelekwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma, kituo cha Afya cha Wilaya Makole na Bahi kwaajili ya kupatiwa matibabu.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule, amefika katika eneo la tukio kujionea hali halisi ya ajali hiyo kabla ya kutembelea majeruhi waliolazwa hospitalini ambapo akiwa hospitalini, amepokea taarifa kutoka kwa wataalamu wa afya kuhusu maendeleo ya matibabu na kujionea huduma zinazotolewa kwa majeruhi.

Imeelezwa kuwa majeruhi wote wamepatiwa matibabu stahiki na hali za wengi wao zinaendelea kuimarika huku wakifuatiliwa kwa karibu na wataalamu wa afya.

Wakati huo huo, vyombo vya ulinzi na usalama vinaendelea na uchunguzi ili kubaini chanzo halisi cha ajali hiyo ambapo taarifa za awali zinaeleza kuwa ezembe wa dereva wa moja wapo ya magari hayo ndio umepelekea kutokea kwa ajali hiyo.

Serikali ya mkoa wa Dodoma imewataka madereva na watumiaji wote wa barabara kuendelea kuzingatia sheria na kanuni za usalama barabarani ili kupunguza ajali zinazogharimu maisha ya watu na kusababisha majeraha.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.