Mfanyabiashara mashuhuri wa Zimbabwe, Wicknell Chivayo amefariki dunia, baada ya helikopta binafsi aliyokuwa akisafiria pamoja na watu wengine watano, kuanguka katika eneo la vijijini la Marondera.
Msemaji wa familia, Herbert Chivayo, amethibitisha kifo cha Chivayo pamoja na mke wake, Lucy Muteke, katika ajali hiyo iliyotokea jioni ya Septemba 30, 2026.

Akizungumza na Shirika la Habari la ZBC, Herbert amesema familia imekumbwa na huzuni na kwamba wanatarajia kuoa taariza zaidi hapo baadaye.
Msemaji wa Polisi ya Zimbabwe, Kamishna Paul Nyathi, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.

Discussion
Reader comments
0 contributions