Na Saulo Stephen - Singida.
Watu sita wamefariki na wengine 55 kujeruhiwa, baada ya basi walilokiwa wakisafiria mali ya Kampuni ya Greenline kupinduka, katika Kijiji cha Mkiwa, kilichopo Wilaya ya Ikungi mkoani Singida.
Basi hilo lililokuwa likitokea Dodoma kuelekea mkoani Mwanza, lilipata ajali wakati likijaribu kukwepa shimo barabarani, jambo lililosababisha dereva kushindwa kulimudu.

Tayari, Jeshi la Polisi mkoani Singida limeanza uchunguzi huku likiwahimiza madereva kuchukua tahadhari wanapopita katika maeneo yenye changamoto za miundombinu, ili kulinda usalama wa abiria na mali zao.
Aidha, Majeruhi wote 55 wamekimbizwa katika Hospitali ya Wilaya ya Manyoni kwa matibabu ya dharura, huku miili ya marehemu ikihifadhiwa katika katika chumba cha maito cha Hospitali hiyo.

Mganga Mkuu wa hospitali ya Halmashauri ya wilaya ya Manyoni, Mkoani Singida, Dkt Bwire James ,amethibitisha kupokea miili sita ya watu waliopoteza maisha katika ajali ya basi hilo lenye namba za usajili T689 DCN.
Akizungumza na Jambo Media kwa njia ya simu Dkt James amesema,"leo asubuhi tumepokea miili ya watu sita waliopoteza maisha na majeruhi hamsini na tano kutoka katika ajali ya basi iliyotokea leo huko mkiwa ,kati ya miili sita hiyo watatu wakike na watatu wa kiume."
Discussion
Reader comments
0 contributions