Skip to main content

AJALI YA BASI MIZA EXPRESS YAUWA WANNE TABORA

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, ACP Twawa Juma Lulengelule amethibitisha kutokea kwa vifo vya watu wanne, wakiwemo Watoto wawili, vilivyosababishwa na ajali ya basi la Kampuni ya Miza Express, lililokuwa likitoka Mpanda kuelekea Bariadi.

Ajali hiyo imetokea katika Kijiji cha Ngukumo, Wilaya ya Nzega Mkoani Tabora majira ya saa 9 usiku, baada ya basi hilo kuacha njia na kutumbukia bondeni, kilomita chache kabla ya kufika Makao Makuu ya Wilaya ya Nzega.

Kamanda amesema, uchunguzi wa awali umebaini kuwa chanzo cha ajali hiyo ni Dereva wa basi hilo kukosa umakini na kushindwa kulimudu na lilitoka nje ya barabara, kugonga vyuma vya kingo za barabara na kisha kupinduka na kutumbukia bondeni.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.