Skip to main content

AJALI MOROGORO: VIFO VYAFIKIA 32, POLISI WAANZA UCHUNGUZI

Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro, linafanya uchunguzi wa tukio la ajali hiyo ya barabarani iliyotokea katika eneo la Kijiji cha Mkambarani, Wilaya na Mkoa wa Morogoro.

AJALI MOROGORO: VIFO VYAFIKIA 32, POLISI WAANZA UCHUNGUZI
Studio Narration JAMBO FM

AJALI MOROGORO: VIFO VYAFIKIA 32, POLISI WAANZA UCHUNGUZI

0:00 --:--

Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro, linafanya uchunguzi wa tukio la ajali hiyo ya barabarani iliyotokea katika eneo la Kijiji cha Mkambarani, Wilaya na Mkoa wa Morogoro.

Ajali hiyo imetokea Oktoba 08, 2026, saa 4 usiku katika Barabara Kuu ya Morogoro-Dar es Salaam, ikihusisha basi lenye namba za usajili T.672 ELT aina ya Higer, mali ya kampuni ya Green Line linalofanya safari zake Mbeya-Dar es Salaam.

Gari hilo, lilikuwa likiendeshwa na dereva aliyefahamika kwa jina la Silaji Athumani Ndosi, na lori lenye namba za usajili T.902 EGN aina ya Scania lenye tela ambalo namba zake hazijafahamika.

Katika safari hiyo, tela lilikuwa limepakia shehena ya mirunda likiendeshwa na Abdallah (36), mkazi wa Makambako Mkoa wa Njombe.

Lori hilo lilikuwa likitokea Iringa kuelekea Dar es Salaam liligongana na basi kisha kuteketea kwa moto na kusababisha vifo vya watu 23 waliokuwa kwenye basi na watu 2waliokuwa kwenye Lori.

Taarifa ya Polisi Mkoani humo inaeleza kuwa, majeruhi ni 30 kutoka kwenye basi ambao walifikishwa katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Morogoro kwa ajili ya matibabu.

Taarifa hiyo inaeleza kuwa, miili ya marehemu imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali hiyo.

Hata hivyo, Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serkali inafanya utaratibu kwa ajili ya kurahisisha utambuzi wa miili ya marehemu kutokana na kuharibika kwa kushirikiana na ndugu zao.

Majeruhi katika ajali hiyo ni Glory Michael, Issa Said, Sapi Raymond, Bruno Waya, Fabiani Aduka, Issaya Richard, Asia Msalanje, Glory Ally, Melata Mgorata, Daniel Malagala, Oliver Paulo, Carolina Thomas, Athuman Pazi na Mohamed Abdalah.

Wengine ni Jane Peter, Abdikadir Liwagala, Mohamed Abdikadiri, Omary Abdikadir, David Paulo, Henry Nyarike, Aman Philipo, Neema Shaban, Consolata Mwalutanile na Sheila Magala.

Wakati huo huo, inaarifiwa kuwa Watu 32 wamefariki dunia na wengine 37 kujeruhiwa katika ajali mbili za barabarani zilizotokea usiku wa kuamkia leo katika maeneo ya Mkambarani na Mvomero, mkoani Morogoro.

Kwa mujibu wa taarifa ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro, vifo 28 vimetokana na ajali ya basi lililogongana uso kwa uso na lori aina ya Scania katika eneo la Mkambarani. Kati ya miili hiyo, 11 bado haijatambuliwa jinsia.

Taarifa zaidi tafadhali angalia kiambata namba 1&2.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.