Skip to main content

AGIZO MATUMIZI YA NIDA: SERIKALI YAKUTANA NA WAMILIKI NYUMBA ZA KULALA WAGENI KAHAMA

Na William Bundala, Kahama - Shinyanga.

AGIZO MATUMIZI YA  NIDA: SERIKALI YAKUTANA NA WAMILIKI NYUMBA ZA KULALA WAGENI KAHAMA

Na William Bundala, Kahama - Shinyanga.

Serikali wilayani Kahama Mkoani Shinyanga, imekutana na wamiliki wa nyumba za kulala wageni na nyumba za kupangisha kwa ajili ya kutoa maelekezo ya matumizi ya Namba za uraia NIDA Pamoja pasipoti za kusafiria kwa wageni katika nyumba hizo.

Akiongea katika kikao hicho, Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wilaya ya Kahama, ambaye ni Mkuu wa Wilaya hiyo, Frank Nkinda amesema kuwa wamiliki na wasimamizi wa nyumba hizo wanatakiwa kuhakikisha watu wote wanaolala katika nyumba hizo wanakuwa na vitambulisho vya NIDA au pasipoti kwa wale wanaotoka nje ya nchi na kwamba wakikosa vitu vyote wawe na utambulisho kutoka katika ofisi ya serikali ya mtaa.

Amesema, "Ndugu wamiliki maagizo ya serikali ni kwamba kuanzia sasa ni marufuku watu kulala kwenye nyumba za kulala wageni bila kitambulisho cha NIDA na wale wanaotoka nje ya nchi wawe na pasipoti hii ni kwasababu ya ulinzi wa wilaya yetu,lakini kama atakosa vitu vyote awe na barua ya utambulisho kutoka ofisi ya serikali ya mtaa.”

Katika hatua nyingine Nkinda amesisitiza mawasiliano kati ya wasimamizi wa nyuma za kulala wageni na kamati ya ulinzi ya kata ili kurahisisha utoaji wa taarifa ikiwa watawapokea watu ambao wana mashaka nao katika nyumba zao za biashara.

“Jambo la pili naomba kusisitiza kuhusu mawasiliano kati ya wasimamizi wa nyumba za kulala wageni na kamati ya ulinzi ya Kata husika akiwemo mwenyekiti wa mtaa na mtendaji wa kata,hawa ndio watu wa kwanza kuwapa taarifa ikiwa mtapokea watu ambao hamuwaelewi katika maeneo yenu,” amesisitiza Nkinda.

Kwa upande wake Meya wa Manispaa ya Kahama, Mataluma Kaniki amewasisitiza wamiliki na wasimamizi wote wa nyumba za kulala wageni kuzingatia maagizo ya serikali ili wafanye kazi bila usumbufu kutokana na ukaguzi wa mara kwa mara utakaofanyika katika maeneo yao ya biashara.

“Ndugu wafanyabiashara wenzangu,niwaombe sana tuzingatie maagizo ya serikali kwa kufuata utaratibu zote ambazo tumeelekezwa,hii itasaidia kufanya kazi bila usumbufu maana ukaguzi ambao utafanyika usipofuata utaratibu utaona kama unasumbuliwa” Amesisitiza Kaniki.

Naye afisa usajili wa mamlaka ya vitamulisho vya taifa (NIDA) manispaa ya Kahama Siriel Mchomvu amesema kuwa wamepokea vitambulisho vingi vya NIDA na kwamba watatumia wiki mbili kuhakikisha kila mwananchi wa halmshauri ya Manispaa ya Kahama,Ushetu na msalala anapata kitambulisho chake na kutoa wito kwa wananchi kufuatilia vitambulisho vyao.

“Kuhusu vitambulisho vya taifa (NIDA) tumepokea vitambulisho vingi na tutatumia wiki mbili kuhakikisha kuwa wananchi wote ambao hawana vitambulisho wanapata vitamulisho vyao,Hivyo niwaomba sana wananchi wote wafatilie vitambulisho vyao kwani kwa sasa kila kitu kinahitaji uwe na kitambulisho,” amesema Mchomvu.

Baadhi wa wamiliki na wasimamizi wa nyumba za kulala wageni, wamesema wamepokea maagizo hayo na watayafanyia kazi na kwamba wanahofia biashara zao kuzorota kutokana na wateja wengi kutokuwa na vitamulisho hivyo.

“Sisi tumepokea kwa utaratibu mzuri maagizo haya ya serikali lakini hofu yetu ni kuzorota kwa  biashara zetu maana wateja wetu wengi hawana vitambulisho wengi wao wana namba tu,sasa tungeomba serikali walitazame hili kwa upande wetu ili nasi tufanye biashara ili tuweze kulipa mapato ya serikali,” wamesema wamiliki hao.

Manispaa ya Kahama ina jumla ya nyumba za kulala wageni zipatazo 400 Kwa mujibu wa takwimu ya mwaka 2025.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.