Skip to main content

AFISA MAENDELEO JELA MIAKA 20, KULIPA MIL. 38 AKIMALIZA KIFUNGO

Na Daniel Gahu - Katavi.

AFISA MAENDELEO JELA MIAKA 20, KULIPA MIL. 38 AKIMALIZA KIFUNGO

Na Daniel Gahu - Katavi.

Hukumu hiyo imesomwa leo tarehe 26/06/2026 mbele ya Mheshimiwa Hakimu Mkazi Mwandamizi Andrea Njau katika Mahakama ya wilaya ya Mlele iliyopo Inyonga ambapo kesi hiyoya Uhujumu Uchumi namba 20135/2025 iliyokuwa ikimkabili.

Shauri hilo limeendeshwa na mwendesha mashtaka wa TAKUKURU John Kitutu ambapo mshtakiwa Bw. PHARES MSILANGA EVARIST- Aliyekuwa Afisa Mtendaji wa kijiji cha Mapili na Utende kwa kipindi cha mwaka 2018 - 2020 Katika Halmashauri ya wilaya Mlele Mkoani Katavi ambapo pia aliwakilishwa na wakili msomi Adv. Gadiel Runyamila Sindamenya.

Mtuhumiwa ametiwa hatiani kwa Makosa matatu, ambapo kosa la kwanza lililomtia hatiani ni kosa la ufujaji na ubadhirifu wa fedha kiasi cha Tshs. 38,391,587/= alizokusanya kama ushuru halali wa Halmashauri ya wilaya ya Mlele, kwa kutumia vibaya mamlaka yake na kuisasabibishia mamlaka hiyo hasara.

Ambapo kitendo hicho ni Kinyume na kifungu Cha 28(1), 31 cha sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa sura ya 329 kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2023 vikisomwa pamoja na aya ya 21 jedwali la kwanza, kifungu cha 57(1) na 60(2) cha Sheria ya uhujumu uchumi na makosa ya kupanga Sura ya 200 marejeo ya 2022.

Kosa la pili ni kosa la matumizi mabaya ya madaraka na kosa la tatu lililomtia hatiani mshtakiwa ni kosa la kuisasabibishia hasara mamlaka ya Halmashauri ya wilaya ya Mlele Mapato, ambapo kinyume na kifungu cha 28(1),31 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Sura ya 329 kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2023.

Vikisomwa pamoja na aya ya 23, jedwali la kwanza kifungu cha 57(1) na 60(2) cha sheria ya uhujumu uchumi na makosa ya kupanga sura ya 200 marejeo ya mwaka 2022.

Aidha kabla ya kusomwa kwa hukumu, Phares Msilanga Evarist alipewa nafasi ya kujitetea ili mahakama tukufu iweze kutoa hukumu isiyokuwa na uonevu, ambapo mshitamiwa alitoa utetezi wa kuwa yeye anategemewa, kwani ana mke pamoja na watoto wawili ambao bado wanahitaji msaada wake wa kimalezi.

Sambamba na hilo Phares Msilanga Evarist aliendelea kuiomba Mahakama impunguzie adhabu kwani ana wazazi wote wawili pamoja na ndugu yake ambaye ni mgonjwa wa tezi dume ambao wote hao bado wanamtegemea kwa asilimia kubwa.

Licha ya utetezi huo mahakama imetoa hukumu kwa mshtakiwa Phares Msilanga Evarist hukumu ya kifungo cha ndani cha miaka 20 jela na kufidia kiasi cha Tshs. 38,391,587/= Mara tu atakapo maliza kifungo chake.

Kwa upande wake Mwendesha Mashtaka wa TAKUKURU John Kitutu aliiomba Mahakama kutoa adhabu kali kwa mshtakiwa huyo ili iwe fundisho kwa watumishi wengine wa Umma kuzingatia maadili, Sheria na taratibu za utumishi wa Umma.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.