Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela, Bi. Ummy Wayay ametangaza kifo cha mtumishi, Bi. Fatuma Shaban Ibrahim aliyekuwa Afisa Habari wa Halmashauri hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Julai 8, 2026 Bi. Fatuma amefariki dunia Julai 7, 2026 majira ya asubuhi akiwa anapata matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando.

Akizungumza kwa njia ya simu, Afisa Habari wa Manispaa ya Ilemela, Violencea Mbakile amesema Mamlaka ya Manispaa ya Ilemela imetoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki wa Bi. Fatuma kwa msiba huo.
Discussion
Reader comments
0 contributions