Skip to main content

AFGHANISTAN: MFUPA MGUMU ULIOMSHINDA FISI 'KILA MTU FUNDI'

Ni nchi moja pekee duniani, ambayo hata mataifa makubwa zaidi yameshindwa kuivamia na kuitawala.

AFGHANISTAN: MFUPA MGUMU ULIOMSHINDA FISI 'KILA MTU FUNDI'

Ni nchi moja pekee duniani, ambayo hata mataifa makubwa zaidi yameshindwa kuivamia na kuitawala.

Nchi hiyo ni Afghanistan.

Wanaiita "Graveyard of Empires".

Afghanistan inaitwa hivyo kwasababu kila himaya iliyojaribu kuingia huko, imetoka ikiwa imevunjika, lakini kwa nini? Si nchi maskini isiyo na bahari?

Hizi hapa sababu 5 zinazoifanya Afghanistan kuwa 'chimbo' gumu kumeza.

1. 'Mchawi' JIografia.

Afghanistan ni nchi ya milima mikali na mabonde marefu. Zaidi ya 75% ya nchi ni milima. Mlima wa Hindu Kush una urefu wa zaidi ya mita 7,000.

Majeshi makubwa yenye vifaru na ndege hayawezi kupita huko. Wanajeshi wa Taliban wanajua kila kichaka, kila pango, na kila njia ya siri.

Ukiwa hapo Mgeni waweza potea, lakini mwenyeji anajua kila njia.

2. Watu Wake Hawajawahi Kukubali Kutawaliwa.

Waafghanistan ni watu wa makabila Pashtun, Tajik, Hazara, Uzbek.

Makabila haya yanaweza kupigana wenyewe kwa wenyewe, lakini mgeni akija, wote wanashirikiana kumpiga mgeni.

Kwao, kupigana ni sehemu ya utamaduni. Mtoto wa miaka 10 anajua kutumia bunduki kuliko askari wa Ulaya.

3. Uingereza Walijaribu Mara 3, Wakashindwa.

Mwaka 1839 hadi 1919, Uingereza ambayo wakati huo ilikuwa himaya kubwa zaidi duniani ilijaribu kuivamia Afghanistan mara 3.

Mara ya kwanza, jeshi la Waingereza la askari 16,000 lilipokuwa likirudi nyuma, liliuliwa wote.

Ni mtu mmoja tu aliyebaki hai kufika Jalalabad. Mmoja tu!

4. Urusi (Soviet) Ilivunjika Huko.

Mwaka 1979, Urusi iliingia na jeshi la kisasa sana. Walidhani itakuwa miezi michache. Ikawa miaka 10 ya mateso.

Wapiganaji wa Mujahideen, wakisaidiwa na Marekani, waliwapiga kwa mbinu za kuvizia milimani.

Urusi ikapoteza askari 15,000, ikatumia mabilioni, na hatimaye ikarudi nyumbani ikiwa imevunjika. Miaka 2 baadaye, Urusi yenyewe ikaanguka.

5. Marekani ilitumia Miaka 20, kaondoka Usiku.

Mwaka 2001, Marekani iliingia baada ya mashambulizi ya 9/11. Ilikuwa na teknolojia kubwa zaidi duniani - drones, satellite, mabomu ya kisasa.

Lakini baada ya miaka 20, trilioni 2 za dola, na askari 2,400 waliokufa, Agosti 2021 Marekani iliondoka usiku, ikiacha ndege, vifaru na silaha. Siku iliyofuata, Taliban wakachukua Kabul bila risasi hata moja.

HITIMISHO:

Afghanistan haiwezi kuvamiwa kwa sababu haina mji mkuu mmoja wa kuteka, haina jeshi moja la kushinda, haina serikali moja ya kubomoa.

Ni milima, makabila, na watu ambao wanapendelea kufa kuliko kutawaliwa.

Kama historia inavyosema: Unaweza kuingia Afghanistan, lakini hutoki kama ulivyoingia.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.