Skip to main content

KAMBI YA MADAKTARI BINGWA WA HUDUMA ZA MACHO YAENDELEA KUWANUFAISHA WANANCHI KARAGWE

Na Clavery Christian, Karagwe - Kagera

KAMBI YA MADAKTARI BINGWA WA HUDUMA ZA MACHO YAENDELEA KUWANUFAISHA WANANCHI KARAGWE

Na Clavery Christian, Karagwe - Kagera

Madaktari bingwa wa macho pamoja na wataalamu wa huduma za macho kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Bukoba, kwa udhamini wa shirika la KCCO, wameweka kambi ya siku tano ya kutoa huduma za kibingwa za macho kwa wananchi wa Wilaya ya Karagwe katika Kituo cha Afya Kayanga kilichopo Wilaya ya Karagwe mkoani Kagera.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuwasili kituoni hapo, Daktari Bingwa wa Macho kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Bukoba, Dkt. Daniel Mashamba, alisema kuwa kambi hiyo imelenga kuwasogezea wananchi huduma za kibingwa za macho karibu na maeneo yao, hususan wakazi wa Wilaya ya Karagwe na maeneo ya jirani.

Alifafanua kuwa katika kipindi chote cha kambi hiyo, wananchi watapatiwa huduma mbalimbali zikiwemo uchunguzi wa macho, ushauri nasaha, utoaji wa dawa, huduma ya miwani pamoja na upasuaji mdogo na mkubwa wa macho kulingana na mahitaji ya mgonjwa.

“Kambi hii ni sehemu ya mkakati wa hospitali wa kuwafikia wananchi moja kwa moja ili kupunguza gharama za usafiri na muda wanaotumia kufuata huduma za kibingwa,” alisema Dkt. Mashamba.

Kwa upande wake, Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Kayanga, Dkt. Wenceslaus Lembekea, aliwakaribisha wananchi wote wa Wilaya ya Karagwe kujitokeza kwa wingi kutumia fursa hiyo muhimu ya huduma za macho.

Dkt. Lembekea alibainisha kuwa kituo kimejipanga kikamilifu kwa kushirikiana na madaktari bingwa hao ili kuhakikisha huduma zinatolewa kwa ufanisi, haraka na kwa kuzingatia viwango vya kitaalamu.

Aliongeza kuwa huduma hizo zilianza rasmi tarehe 08 Juni 2026 kuanzia saa 2:00 asubuhi na zinatarajiwa kuhitimishwa siku ya Ijumaa tarehe 12 Juni 2026.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.