Shambulio la kombora ambalo limetekelezwa na Urusi mjini Kramatorsk mashariki mwa Ukraine limesababisha vifo vya watu 33 na makumi kujeruhiwa.
Mamlaka za Ukraine zimesema mapema leo oct.8 kwamba, shambulio hilo ni lakimakusudi dhidi ya raia katika eneo hilo lenye kuwekwa shabaha kwa muda mrefu na Moscow.

Katika taarifa ya awali mamlaka za Ukraine zimeeleza kuwa Watu wapatao 18 wamejeruhiwa katika shambulio hilo lilitokea katika mtaa ambapo mabasi mawili ya mji huo yalikuwa yakifanya kazi kabla ya kombora kutua.
Rais Volodymyr Zelenskiy wa Ukraine ameeleza eneo hilo kuwa ni kituo cha mabasi, huku Picha zilizochapishwa na jeshi la polisi zilionesha miili ya wahanga ikiwa imetapakaa mtaani katikati ya vifusi, pamoja na mabaki ya basi lililoungua kabisa kwa moto.
Gavana wa Mkoa wa Donetsk, Vadym Filashkin, kupitia mtandao wa Telegram, amelaani vikali shambulio hilo akisema kuwa jeshi la Urusi limefanya hivyo kwa kunuia kuuwa watu kwa alaiki.

Kufuatia mripuko huo, Gavana Filashkin ameamuru mamlaka za miji ya Kramatorsk na Sloviansk kusitisha mara moja huduma zote za usafiri wa umma, akisisitiza kuwa serikali haina haki ya kuendelea kuhatarisha maisha ya raia.
Shambulio jilo limejiri siku moja baada ya mashambulio mengine makubwa ya angani kuarifiwa kuua makumi ya watu nchini Ukraine, yakilenga zaidi mifumo ya umeme..
Hadi sasa hakuna tamko rasmi lililotolewa na Moscow kuhusu shambulio hilo. hapo awali Urusi iliitaka Ukraine isalimishe maeneo yote yaliyosalia ya mkoa huo yanayodhibitiwa na Kyiv kabla ya kusitisha vita, sharti ambalo serikali ya Ukraine imelikataa kata kata.
Discussion
Reader comments
0 contributions