Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza, linawashikilia kwa mahojiano watu 23, kwa tuhuma za kupanga njama za kufanya vurugu na uhalifu katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Mwanza wakati wa madhimisho ya Sababasa.
Watu hao, walikamatwa kati ya Julai 5 hadi 7 2026, kupitia doria za kawaida zilizofanywa na Polisi katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Mwanza.

Miongoni mwa waliokamatwa ni wakazi wa maeneo ya Gedeli, Nyakato, Igoma, Gana, Pansiasi, Bwiru na Nyambiti, kutoka Manispaa za Ilemela na Nyamagana.
Kwa mujibu wa taarifa ya Polisi, uchunguzi wq tuhuma hizo bado unaendelea na wale watakaothibitika kuhusika na makosa hayo watafikishwa mahakamani.
Discussion
Reader comments
0 contributions