Skip to main content

23 KORTINI KWA TUHUMA UGAIDI MWANZA

Watu 23 wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mwanza na kusomewa shtaka moja la kushiriki kwenye mikutano ya kigaidi.

23 KORTINI KWA TUHUMA    UGAIDI MWANZA

Watu 23 wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mwanza na kusomewa shtaka moja la kushiriki kwenye mikutano ya kigaidi.

Waliopandishwa kizimbani ni Alphaxad Nyamwaga (57), Fantson Mpango (49), Abely Mwesa (62), Hassan Said (43), Emmanuel Wambura (30), Adam Idd (23), Damas Sadock(31), Petrol Mabula (40), Abdul Kagwidi (28), Devid Mahendeka (20), Philipo Masatu (31), Edward Mikindo (28) na Emmanuel Doto (26).

Wengine ni Deus Masalago (41), Mohamed Tosha (37), Fabian Nguvumali (52), Samwel Mtani (45), Samwel Kobell (40), Julius Makonga (34), Fanuel Lutana (35), Philipo Kulwa (37) , Philipo Shipuluko (50) na Hamis Mnyivua (35).

Washtakiwa hao wanadaiwa kutenda makosa hayo kati ya Julai 4, na Julai 7 mwaka huu, katika wilaya za Nyamagana na Ilemela mkoani humo.

​Washtakiwa wamefikishwa mahakamani leo, Julai 23, 2026, chini ya ulinzi mkali wa Jeshi la Polisi na kusomewa shtaka linalowakabili kwa nyakati tofauti na kwa makundi kulingana na maeneo wanakodaiwa kutenda makosa hayo, katika Kesi Namba 16375 ya mwaka 2026 na 16377 ya mwaka 2026.

​Akisoma shtaka hilo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mwanza Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Mwanza, Mheshimiwa, Erick Marley, Kiongozi wa Jopo la Waendesha Mashtaka wa Serikali, likiongozwa na Joseph Maugo Wakili mkuu wa Serikali na mkuu wa mashtaka mkoa wa Mwanza.

Wote walikuwa wakisaidiana na Janess Kihwelo wakili wa serikali mwandamizi, Sileo Muzullah wakili wa serikali pamoja na Evance Kaiza wakili wa serikali, amesema shtaka linalowakabili washtakiwa 13 kutoka Wilaya ya Ilemela ni kutenda kosa la kushiriki kwenye mikutano ya kigaidi.

Kwa mujibu wa jopo hilo, washtakiwa hao walitenda makosa hayo kinyume na kifungu cha 4(1)(2)(a), 5(a) na 12(1)(c) cha Sheria ya Kuzuia Ugaidi, Sura ya 19 Toleo la 2023, ikisomwa pamoja na aya ya 24 ya Katiba na vifungu vya 57(1) vya Sheria ya Udhibiti wa Makosa ya Kiuchumi na Uhalifu Uliopangwa, Sura ya 200 Toleo la 2023.

​Washtakiwa wengine 10 kutoka Wilaya ya Nyamagana wamesomewa shtaka hilo wakidaiwa kufanya vitendo hivyo katika eneo la Igoma jijini Mwanza.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.