Skip to main content

180 WAFANYIWA UPASUAJI WA MACHO SINGIDA, MAELFU WAPATA HUDUMA

Huduma za uchunguzi wa afya ya macho zimetolewa kwa wananchi 1,500 mkoani Singida, huku wananchi 180 wakifanyiwa upasuaji wa mtoto wa jicho katika wiki ya maadhimisho ya Siku ya Afya ya Macho Duniani.

180 WAFANYIWA UPASUAJI WA MACHO SINGIDA, MAELFU WAPATA HUDUMA
Studio Narration JAMBO FM

180 WAFANYIWA UPASUAJI WA MACHO SINGIDA, MAELFU WAPATA HUDUM...

0:00 --:--

Huduma za uchunguzi wa afya ya macho zimetolewa kwa wananchi 1,500 mkoani Singida, huku wananchi 180 wakifanyiwa upasuaji wa mtoto wa jicho katika wiki ya maadhimisho ya Siku ya Afya ya Macho Duniani.

Mratibu wa Huduma za Macho Mkoa wa Singida, Dkt. Upendo Mwakabalile, amesema hayo wakati akiwasilisha taarifa ya utoaji wa huduma za macho katika maadhimisho yaliyofanyika kitaifa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida Mandewa.

Amesema Mkoa wa Singida ulifungua vituo vitatu vya utoaji huduma za uchunguzi na upasuaji wa macho, ambapo Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida ilifanya uchunguzi kwa wananchi 400 na upasuaji wa mtoto wa jicho kwa wananchi 30.

Ameongeza kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Singida Vijijini ilifanya uchunguzi kwa wananchi 500 na upasuaji wa mtoto wa jicho kwa wananchi 55, huku Kituo cha Afya Ihanja kilichopo Ikungi kikifanya uchunguzi kwa wananchi zaidi ya 600 na upasuaji kwa wananchi 100.

Akizungumza katika maadhimisho hayo, Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Singida, Lussa Kitiku, amesisitiza kuwa utunzaji wa macho ni jukumu la kila mmoja na kuwataka wananchi kuacha kukaa na matatizo ya uoni majumbani badala ya kufika katika vituo vya kutolea huduma za afya ya macho.

Amesema ni muhimu kila mmoja kuwa balozi wa utunzaji wa macho nyumbani na mitaani, huku akiipongeza Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali katika kuboresha miundombinu na huduma za kibingwa za macho.

Aidha, amewapongeza wananchi waliojitokeza kupima afya zao na kuwakumbusha umuhimu wa kupima afya ya macho angalau mara moja kwa mwaka au pale wanapoelekezwa na wataalamu wa afya.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.