Skip to main content

149 WAKAMATWA KWA MAKOSA MBALIMBALI MARA

Na Adam Msafiri - Mara.

149 WAKAMATWA KWA MAKOSA MBALIMBALI MARA

Na Adam Msafiri - Mara.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mara, limewakamata watuhumiwa 149 wa makosa mbalimbali ya uhalifu katika kipindi cha mwezi Juni hadi Julai 2026 kupitia oparesheni na misako iliyoendeshwa katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo.

Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Pius Lutumo amesema kati ya watuhumiwa hao, watu 85 wamefikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili, huku washitakiwa watano waliokamilisha kesi zao wakitiwa hatiani na kuhukumiwa vifungo vya jela.

Kamanda Lutumo amesema mafanikio hayo yametokana na juhudi za Jeshi la Polisi katika kuimarisha doria, kufanya oparesheni za mara kwa mara pamoja na ushirikiano mzuri kutoka kwa wananchi wanaotoa taarifa za uhalifu kwa wakati.

Aidha, ameeleza kuwa hali ya usalama katika Mkoa wa Mara inaendelea kuwa tulivu, akibainisha kuwa Jeshi la Polisi litaendelea kusimamia sheria kwa weledi na kuwachukulia hatua wote watakaobainika kujihusisha na vitendo vya uhalifu.

Amewahimiza wananchi kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa zinazoweza kusaidia kuzuia na kudhibiti uhalifu ili kuendelea kudumisha amani na usalama katika Mkoa wa Mara.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.