NETANYAHU ATISHIA KUANZISHA UPYA MAPIGANO GAZA

Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu ametishia kuvunja makubaliano ya kusitisha mapigano na kuanza tena vita dhidi ya Gaza.

Kauli ya Netanyahu anaitoa huku akidai hayo yatatimia ikiwa Hamas haitawaachilia mateka watatu wanaowataka hadi kufikia Jumamosi ya Februari 15, 2025.

Amesema, makubaliano yao ya kusitisha mapigano ambayo yalianza Januari 19, 2025 yametiliwa shaka baada ya maafisa wa Hamas kusema kuwa Israel imekiuka masharti muhimu.

Jambo hilo limesababisha kundi la Hamas kusitisha kuwaachia mateka watatu waliopaswa kuachiwa Jumamosi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *