Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) limetangaza matokeo ya Mtihani wa kidato cha sita uliofanyika Mei 5 – 26, 2025 na kueleza kuwa Watahiniwa wa Shule 2025 waliofaulu ni 125, 779 sawa na asilimia 99.95.
Matokeo hayo yametangazwa hii leo Julai 7, 2025 visiwani Zanzibar na Katibu Mtendaji wa NECTA, Prof. Said Mohamed ambaye amesema Watahiniwa walioshindwa mtihani ni 68 sawa na asilimia 0.05.
Amesema “NECTA imefuta matokeo yote ya Watahiniwa 71 wakiwemo 70 wa Mtihani wa Kidato cha Sita (64 wa Shule na 6 wa Kujitegemea) na mmoja wa Mtihani wa Ualimu Daraja A (GATCE) baada ya kubainika kufanya udanganyifu katika Mtihani.”

“Matokeo hayo yamefutwa kwa mujibu wa Kifungu cha 5 (2) (i) na (j) cha Sheria ya Baraza la Mitihani Sura ya 107 kikisomwa pamoja na Kifungu cha 30(2) (b) cha Kanuni za Mitihani za Mwaka 2016,” alisema Dkt. Said.
Kuona matokeo yote ya Midato cha sita tafadhali fungua link hapo chini.


