Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Nduguru amewataka wakuu wa shule za msingi kuwalinda watoto dhidi ya ukatili wa kijinsia

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Adolf Ndunguru amewataka walimu wakuu wa shule za msingi kwa kushirikiana na Wakurugenzi wa Halmashauri kuweka mifumo na mikakati maalumu ili kuwalinda watoto dhidi ya matukio ya ukatili wa kijinsia ambayo yamekuwa yakitokea katika jamii.

Ndunguru ameyasema hayo wakati akifunga mafunzo ya ujenzi na usalama wa mazingira yaliyokuwa yakitolewa kwa walimu wakuu wa shule za msingi na maofisa mazingira ambayo yamefanyika kwa siku tatu mkoani Mwanza ambapo amesema katika jamii kumekuwa na vitendo vya ukatili wa kijinsia ambavyo vimekua vikifanywa dhidi ya watoto hivyo ni lazima uundwe mfumo na mkakati maalumu wa kuwalinda watoto hao na kutaka vilabu vya wanafunzi kuendelezwa ili kuwajengea uwezo wa kujitambua na kujiamini.

Sambasamba na hayo Ndunguru amesema katika mwaka wa fedha 2023/2024 zaidi ya shilingi bilioni 81 zimepokelewa kutoka serikalini kwa ajili ya ujenzi wa shule mpya za msingi 78, vyumba vya madarasa 1,625, matundu ya vyoo 3,635, nyumba 10 za walimu pamoja na ukarabati wa shule 42.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *