Mahakama kuu ya Tanzania Masijala Kuu Dodoma, imetoa hukumu kwamba Luhaga Mpina hatoweza kuendelea na mchakato wa kampeni za kuwania nafasi ya Urais kupitia tiketi ya chama cha ACT-Wazalendo.
Wakili Kiongozi kwenye Jopo la Mawakili wanoamteta Mpina, John Seka amesema Mahakama imeamua kutupilia mbali madai ya kiongozi huyo pamoja na Chama chake, ikisema kwamba madai yao hayana msingi kutokana na jinsi shauri hilo livyofunguliwa.
Aidha, Mahakama imesema haina uwezo wa kuhoji kile kinachamuliwa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC).

“Kwa mujibu wa katiba Mamlaka ya kuhoji yale yaliofanywa na tume sio mambo yanayoweza kuamuliwa mahakamani na mambo yanayoamuliwa na Tume lazima yaishiye ndani ya Tume,” alisema.
“Njia yake ya kuwania urais ni kama imefungwa kwasasa na sisi tulikuwa tukimpambania aweze kurejeshwa,” aliongeza Ameongeza Wakili Kiongozi Seka.
Hata hivyo, Mahakama imefafanua kwamba Tume ilikuwa na uamuzi wa kumuonoda mpina katika Kinyang’anyiro hicho, uamuzi ambao Seka anasema hawakutegema na kwasasa wanasikiliza ikiwa ACT Wazalendo watahitaji kukata Rufaa.

“Tuseme tu kwamba Mahakama imetekeleza uamuzi wake na sisi tutatekeleza wajibu wetu” Alisema John Seka…amesema siku zilizobaki kukata rufaa zipo ndani ya siku Thelathini za kukata Rufaa, lakini muda huo hautoshi kusikiliza rufaa hiyo,” alisema Seka.
Awali hukumu hiyo ilipangwa kutolewa Oktoba 10, 2025 lakini Mahakama iliomba muda wa ziada, ili kuja na uamuzi usio na shaka.


