Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Ndoa ya Cardi B na Offset ni haipo sawa

Rapa Cardi B na mumewe Offset, wameamua kupunguzana kwenye mtandao wa Instagram (unfollow). Ambapo kila mmoja amefanya hivyo kwa mwenzake.

Hii imekuja baada ya Cardi B kuandika jumbe tata kwenye Instastory yake siku ya jana (Desemba 4) ambapo alianza kwa kuandika “Unajua unapoanza tu kukuza uhusiano,” akaongeza, “Nimechoka kulinda hisia za watu…NI LAZIMA NIJIWEKA MIMI KWANZA.”

Hii si mara ya kwanza  wawili hao kujitokeza hadharani kuonyesha wamezinguana. Utakumbuka Desemba 2018 waliachana baada ya Offset kudaiwa kumsaliti mkewe na wakati huo tayari walikuwa na mtoto mmoja, Ila baada ya miezi miwili walirudiana.

Septemba 2020 Cardi B alienda Mahakamani kuomba taraka yake, Ilipofika Desemba 2020 waliamua kurudiana.

Juni 2023 Offset alimtuhumu mkewe kutokuwa mwamininu kwenye ndoa yao na ikadaiwa wametangana, Julai 2023 Offset aliomba radhi na kusema sio kweli alichosema kwa mkewe.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *