Ndoa ikikushinda, muache ataolewa tena

Naibu Waziri wa Katiba na Sheria na Mbunge wa Jimbo la Babati Pauline Gekul amewashauri Vijana kutoingia katika ndoa kama Majukumu ya ndoa hawayajui ili kupunguzia adhabu wakina mama kulea watoto bila Baba.

Gekul ametoa ushauri huo wakati akizungumza na wananchi wa Mtaa wa Gendi Babati mkoani Manyara, ambapo amesema kuwa mwanaume kama ndoa imemshinda ni Bora wakaachane mahakamani ili mwanamke aolewe na mwanaume mwengine kuliko kumtelekeza na kumuongezea Majukumu mwanamke pasipo na sababu.

Aidha ametoa ushauri kwa wanawake kuwa na cheti Cha ndoa ili wakiachana au mume akifariki awe Sehemu ya kupewa mirathi ambayo ni haki yake ya msingi kwani kuishi na mwanaume bila ndoa na kutokuwa na cheti kutamfanya akose haki zake za msingi kama mke.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *